Kiongozi msimamizi wa BF SUMA, Juma Mwesigwa akiwa katika ofisi za BF SUMA Manispaa ya Shinyanga
Kampuni ya BF SUMA Tanzania inayozalisha bidhaa mbalimbali zinazotibu magonjwa yasiyoambukiza itaendesha semina inayofundisha masuala ya biashara katika Manispaa ya Shinyanga.
Semina hiyo inatarajiwa kufanyika kesho Jumapili ya Disemba 01, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa KARENA HOTEL.
Kiongozi msimamizi wa BF SUMA, Juma Mwesigwa amesema leo Novemba 30, 2024 kuwa semina hiyo inajulikana kwa jina la “AFYA YANGU, UCHUMI WANGU” na semina hiyo ni kubwa kwani wananchi wote ambao wako tayari kushiriki wanakaribishwa na hakuna kiingilio cha kushiriki semina hiyo.
Amesema semina hiyo itahusisha madaktari wabobezi wa magonjwa yasiyoambukiza, kutakuwa na vipimo vinavyopima magonjwa yote yasiyoambukiza pamoja na bidhaa za kampuni hiyo zinazotibu magonjwa yote yasiyoambukiza.
Mwesigwa amesema kila mshiriki wa semina hiyo atapata fursa ya kupima magonjwa yasiyoambukiza kwa hiari na kampuni ya BF SUMA ni kampuni ambayo inazalisha bidhaa bora na ni bora kwa matumizi ya binadamu na huleta mabadiliko kwenye mwili.
“Bidhaa zipo za kutosha kwa magonjwa yote yasiyoambukiza ambayo ni kisukari, saratani, vidonda vya Tumbo, mifupa, Pingili za Mgongo, Bawasili, Presha na magonjwa mengine mengi ikiwemo uzazi kwa wanawake, uzazi kwa wanaume na nguvu za kiume”. amesema.
Madam Lilian akiwa ofisi za BF SUMA pia anahusika na utoaji huduma wa bidhaa
Aidha kiongozi msimamizi wa BF SUMA, Juma Mwesigwa amesema kampuni hiyo imefungua ofisi katika Manispaa ya Shinyanga mjini katika jengo la shirika la nyumba la taifa NHC ghorofa ya nne.
Jengo la NHC zilipo ofisi za BF SUMA Manispaa ya Shinyanga
Kwa mawasiliano Zaidi BF SUMA 0784 150 950
No comments:
Post a Comment