MTOTO WA MIAKA MIWILI ADAIWA KUMWAGIWA MAJI YA MOTO NA BABA WA KAMBO-KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 6 June 2024

MTOTO WA MIAKA MIWILI ADAIWA KUMWAGIWA MAJI YA MOTO NA BABA WA KAMBO-KAHAMA




NA NEEMA NKUMBI HUHESO FM-KAHAMA


Mtoto wa miaka miwili jina tunalo mkazi wa mtaa wa shunu kata ya nyahanga manispaa ya kahama mkoani shinyanga amelazwa katika hospital ya manispaa hiyo kwa madai kuwa amemwagiwa Maji ya moto na baba yake wa kambo anayejulikana kwa jina la Simon Hamisi.


Akisimulia tukio hilo mama mzazi wa mtoto huyo Elizabeth Mathias mbele ya wandishi wa habari katika wodi alikolazwa mtoto huyo amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa mbili usiku alipokuwa akichemsha maji jikoni ndipo mumewe alianzisha mzozo na kulipiga teke jiko ambalo lilikuwa na sufuria la maji ya moto na kummwagikia mtoto wake ambae alikuwa amekaa karibu na jiko hilo.


Aidha Mwanamke huyo amesema kuwa tukio hilo linatokana na ulevi na kufafanua kuwa mumewe hajawahi kufanya tukio lolote baya kwa mwanae alimpenda sana lakini anashangaa kwa kilichotoke.


Katika hatua nyingine mzazi huyo anaiomba serikali kumpa msaada wa matibabu kwani pesa aliyokuwa nayo ametumia kununua dawa na haijatosheleza matibabu pia mume wake tayari ameshikiliwa na polisi.

"Tangu tumekuja ustawi wa jamii humu mwanangu amechomwa sindano moja tu zingine mpaka hela nami sina bora wanisaidie mwanangu apone suala la kula nitahangaika kuwatafuta ndugu zangu wa mwanza" alisema mwanamke huyo.


Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo pia amelaani kitendo cha wazazi kutumia ulevi kufanya matukio ya kikatili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso