WAZIRI UMMY APIGA MARUFUKU UUZAJI WA DAWA YA AMOXICILLIN KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 22 May 2024

WAZIRI UMMY APIGA MARUFUKU UUZAJI WA DAWA YA AMOXICILLIN KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO

Waziri  wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa onyo kwa baadhi ya wahudumu wa afya wanaouza dawa za Amoxicillin DT kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakati wanapoenda kupatiwa matibabu ambapo dawa hizo kwa maelekezo ya Serikali hutolewa bure.

Waziri  wa Afya, Ummy Mwalimu


Waziri Ummy ametoa agizo hilo mkoani Tanga wakati akikabidhi gari ya kubebea wagonjwa ‘Ambulance’ katika kituo cha afya Duga kilichopo Jiji la Tanga ambapo amebainisha kuwa gari hilo ni miongoni mwa Magari zaidi ya 600 yanayosambazwa nchi zima na wizara ya afya kwa kushirikiana na ofisi ya Rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa ‘TAMISEMI’ lengo likiwa ni kutokomeza vifo vya wagonjwa wakiwemo wajawazito wanapohitaji huduma za dharura.


“Lengo letu ni kuboresha huduma za rufaa kwa wagonjwa tunataka tusipoteze watu kwa sababu wagonjwa walikuwa wanafariki kwa sababu ya kukosa huduma kwa wakati hususani wagonjwa wa dharura” amesema Waziri Ummy


Akizungumzia changamoto ya dawa zinazouzwa kinyume na maelekezo ya Serikali , Waziri Ummy amewataka wahudumu wa afya kuzingatia sera ya afya bure kwa  wamama wajawazito na watoto.


“Kama dawa zipo hamna haja ya kumwambia mgonjwa changia zingatieni sera ya matibabu kwa wamama  wajawazito na watoto waliopo chini ya miaka mitano , nimeangalia daftari la wagonjwa kati ya 10 watoto waliokuja hospital 7 wana maambukizi ya Bakteria ambayo inatibiwa na dawa inaitwa Amoxicillini DT, amesema Waziri Ummy


“Dawa hii ya a Amoxicillin DT haipaswi kuuzwa kwa watoto waliopo chini ya miaka mitano na hili nalisisitiza tuzingatie maelekezo ya Serikali , kwa sababu tumeona inauzwa mwaka huu tutaandika haiuzwi sasa ole wake tuikute kwenye  Duka  inauzwa utatuambia umeitoa wapi”  amesema Waziri Ummy

 

Katika kulidhibiti hilo waziri Ummy amesema watatoa semina elekezi kwa viongozi  kuanzia ngazi za vijiji na vitongoji ili kutokomeza tabia hiyo ya baadhi ya watoa huduma ikiwemo maduka ya dawa kuuza dawa ambazo Serikali imeelekeza zitolewa bure kwa wagonjwa.

 

“Itabidi tuende mpaka ndani tuweke alama utakapoona hii dawa imeandikwa GOT ukiiona jua kuwa imeibiwa na haipaswi kuuzwa hizi dawa zinanunuliwa na Serikali na kusambaza hii ndio sera ya matibabu bure” amesema Waziri Ummy

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso