SERIKALI YAPONGEZWA KWA UJENZI WA BARABARA MKOANI MOROGORO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 4 March 2024

SERIKALI YAPONGEZWA KWA UJENZI WA BARABARA MKOANI MOROGORO



MBUNGE wa Jimbo la Gairo, mkoani Morogro, Ahmed Shabiby ameipongeza serikali kwa kutoa fedha za kuanza kufanya usanifu wa barabara ya kutoka Gairo mjini hadi Nongwe yenye urefu wa kilometa 55 ijengwe kwa kiwango cha lami.


Kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango cha lami kutachochea kuinua uchumi wa wananchi wa Wilaya ya Gairo kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara likiwemo zao la kimkakati la parachichi.


Shabiby ametoa pongozi hizo kwenye mkutano na wananchi mbele ya Waziri wa ujenzi , Innocent Bashungwa alipotembelea wilayani humo.


“Nikupongeze mheshimiwa Waziri ulikubali ombi langu na sasa hivi nafiriki kazi imeshatangazwa kufaya usanifu wa kuchora ramani ya barabara ya kutoka Gairo mjini kwenda Nongwe yenye urefu wa kilometa 55,” amesema Shabiby.


“ Nimeona Meneja wetu wa Tanroads mkoa ameshatangaza na anatafutwa mshauri elekezi ili barabara hii iweze kuingizwa kwenye bajeti kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami kutoka Gairo mpaka Nongwe,“ amesema Shabiby.


Shabiby amesema tarafa ya Nongwe iliyopo kwenye safu ya milimani wananchi wake ni wazalishaji mkubwa wa mazao ya aina mbalimbali likiwemo zao la kimkakati la parachichi.


“ Nisema tarafa ya Nongwe ni eneo la uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara na kwa sasa tunazao la kimkakati la Parachichi na vipo vitalu wenye miche zaidi ya 300,000 kwa ajili ya kilimo hiki ,” amesema Shabiby.


chanzo:habarileo.co.tz

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso