TAKUKURU SHINYANGA YASHIRIKIANA NA WADAU SEKTA ZA UMMA KUZIBA MIANYA YA RUSHWA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 1 December 2022

TAKUKURU SHINYANGA YASHIRIKIANA NA WADAU SEKTA ZA UMMA KUZIBA MIANYA YA RUSHWA.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoa Shinyanga (TAKUKURU),imetoa taarifa ya utendaji kazi katika kipindi cha robo mwaka wa fedha (2022/2023)(Julai-septemba,2022)ambapo ilijikita kwenye kuziba mianya ya rushwa na kufanya uzuiaji hasa kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa Mkoani humo.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy  akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 1,2022

NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital SHINYANGA.


Akizungumza na waandishi wa habari leo,Desemba mosi 2022,Mkuu wa TAKUKURU Shinyanga,Donasian Kessy,ameeleza namna walivyofanya kazi katika kipindi hicho.


Kessy,amesema katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo TAKUKURU Mkoa Shinyanga,ilishirikiana vyema na watendaji wa Halmashauri zote za Mkoa wanaohusika na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Ambapo ufuatiliaji ulihusisha kazi za kutembelea miradi na shughuli za ujenzi katika miradi ili kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa inakuwa na thamani halisi na ubora unaotakiwa.


Vilevile,TAKUKURU Shinyanga imeendelea kushIrikiana na wadau wa Halmashauri ili kuhakikisha kuwepo na mazingira mazuri ya kufanyia biashara,Mazingira hayo ni pamoja na kupangisha vibanda vya biasharakwa wafanyabiashara kwa bei nafuu.


Katika eneo la kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoani humo,ilifanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha katika miradi ya maendeleo (28),yenye thamani ya Bil.11.5,iliyotolewa fedha na serikali.


Aidha TAKUKURU imebaini kuwepo kwa Dosari zilizopatikana wakati wa ufuatiliaji wa miradi katika sekta husika zilirekebishwa kwa kutoa elimu na ushauri kwa wadau kuzingatia ubora wa mradi kwa mujibu wa BOQ na baadhi ya dosari zimefanyiwa kazi na zingine zinaendelea kufanyiwa kazi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso