LHRC YAISHAURI SERIKALI MSWADA WA SHERIA UTAKAOJADILIWA NA BUNGE LA 12 UTAZAMWE UPYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 31 October 2022

LHRC YAISHAURI SERIKALI MSWADA WA SHERIA UTAKAOJADILIWA NA BUNGE LA 12 UTAZAMWE UPYA



Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Anna Henga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 31, 2022.



KITUO Cha Haki Za Binadamu kimetoa wito kwa Serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kutazama upya na kwa jicho la pili Miswada ya sheria itakayojadiliwa na kupitishwa katika Mkutano wa Nne wa Bunge la 12.


Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Wakili Anna Henga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 31, 2022.

Miswada hiyo ni Mswada wa Bima ya Afya kwa Wote 2022, Mswada wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi 2022, Mswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali.

“Tunaitaka serikali Pamoja na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvitazama upya vifungu vyote vinavyompa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya afya kutunga kanuni ili kuondoa uwezekano wa kukinzana kwa sheria mama na kanuni kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia siku za hizi karibuni kwenye baadhi ya sheria baada ya kupitishwa na bunge.

Pia Kukifuta kifungu cha 32 kinachoweka zuio la baadhi ya huduma kwani ni kinyume na haki za binadamu.” Amesema Anna

Mswada wa Bima ya Afya kwa Wote 2022

Amesema mswada huu una vifungu tata na vinavyoweza sababisha uvunjifu wa haki za binadamu au kusababisha changamoto katika utekelezaji wake

Kwa upande wa Mswada wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi 2022, wameomba Kuondoa sharti la usajili wa lazima kwa taasisi binafsi zinazojihusisha na ukusanyaji, uchakataji na udhibiti wa taarifa binafsi kwani tayari taasisi hizo zimekwisha sajiliwa kwa mujibu wa sheria nyingine kama vile Sheria ya Makampuni na Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Kupunguza kiwango cha juu cha faini kutoka billion 5 mpaka million 500

Kuhusu Mswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 2022 amesema kuwa Serikali
iachane na dhana ya usajili wa watafiti kwani iko kinyume na katiba haya ibara ya 18 inatoruhusu uhuru wa kupata na kutafuta Habari. Pia usajili wa watafiti itaminya upatikanaji wa taarifa huru za Tanzania ambazo nyingine zinahitajika na watu wanaotaka kuwekeza Tanzania. Tume ya Sayansi na Teknolojia ibaki na majukumu yake ya awali na tafiti ziwe huru.

Kuhusu Mswada wa Bima ya Afya kwa Wote 2022

Tunaitaka serikali Pamoja na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvitazama upya na kwa jicho la pili vifungu vyote vinavyompa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya afya kutunga kanuni ili kuondoa uwezekano wa kukinzana kwa sheria mama na kanuni kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia siku za hizi karibuni kwenye baadhi ya sheria baada ya kupitishwa na bunge.

Pia wametaka Kukifuta kifungu cha 32 kinachoweka zuio la baadhi ya huduma kwani ni kinyume na haki za binadamu.

Mswada wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi 2022

Kuondoa sharti la usajili wa lazima kwa taasisi binafsi zinazojihusisha na ukusanyaji, uchakataji na udhibiti wa taarifa binafsi kwani tayari taasisi hizo zimekwisha sajiliwa kwa mujibu wa sheria nyingine kama vile Sheria ya Makampuni na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Kupunguza kiwango cha juu cha faini kutoka billion 5 mpaka million 500

Kuhusu Mswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 2022
Kuachana na hii dhana ya usajili wa watafiti kwani iko kinyume na katiba haya ibara ya 18 inatoruhusu uhuru wa kupata na kutafuta Habari. Pia usajili wa watafiti itaminya upatikanaji wa taarifa huru za Tanzania ambazo nyingine zinahitajika na watu wanaotaka kuwekeza Tanzania. Tume ya Sayansi na Teknolojia ibaki na majukumu yake ya awali na tafiti ziwe huru.

Kuhusu Mswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 2022
Kuachana na hii dhana ya usajili wa watafiti kwani iko kinyume na katiba haya ibara ya 18 inatoruhusu uhuru wa kupata na kutafuta Habari. Pia usajili wa watafiti itaminya upatikanaji wa taarifa huru za Tanzania ambazo nyingine zinahitajika na watu wanaotaka kuwekeza Tanzania. Tume ya Sayansi na Teknolojia ibaki na majukumu yake ya awali na tafiti ziwe huru.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso