Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema katika kila watoto 100 wenye umri chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Iringa, 47 wamedumaa kutokana na lishe duni.
Amesema japo mkoa huo una kila aina ya chakula suala la lishe kwa watoto bado ni changamoto.
Akizungumza katika wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye jimbo la Isimani, Ummy amesema kiuhalisia watoto waliodumaa hawawezi kufanya vizuri kwenye masomo hata kama Serikali imewekeza kwenye elimu bila malipo.
“Ndugu zangu wana Iringa tunapovua samaki tusiuze wote, tuwape lishe watoto. Hizi mboga za majani wapatie na watoto wetu, Iringa kuna kila aina ya chakula lakini hali ya lishe ni mbaya,” amesema Ummy.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Salim Asas amewataka wakazi wa Iringa kuacha kuwapatia watoto wao ulanzi na badala yake, wawapatie maziwa na vyakula vingine vyenye lishe.
No comments:
Post a Comment