MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewatahadharisha wale wote wenye nia ovu ya kujipatia huduma ya maji kwa njia isiyokuwa halali (kuiba) kuacha haraka iwezekanavyo kwani Serikali haipo tayari kufanya utetezi kwa aina ya mtu huyo, na badala yake itamchukulia hatua za kisheria ikiwemo kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.
RC Macha ameyasema hayo leo Aprili 14, 2025 alipokuwa akiongea na watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) ambao walifika katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwenye hafla ya kukabidhi Magari mawili (2) mapya yenye thamani ya takribani Milioni 276 yenye lengo la kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka hiyi SHUWASA.
"Serikali haipo tayari kabisa kumtetea mtu yeyote na wala haitakuwa na muhali kwa mwananchi yeyote mwenye nia ovu ya kujipatia huduma ya maji kwa njia isiyokuwa halali, na badala yake itamchukulia hatua za kisheria ikiwemo kumfikisha Mahakamani ili iwe mfano kwa yeyote asiyeitakia mama Mamlaka," amesema RC Macha.
RC Macha akiwa ameambatana na ndugu David Lyamongi ambaye aliyemuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni ametumia nafasi hiyo kuipongeza Menejimenti ya SHUWASA inayoongozwa na Mhandisi Yusuph Katopola na watumishi wote kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi kwa asilimia 95 Mjini na 85 kwa maeneo ya Vijijini huku pongezi zaidi ni kwa utekelezaji wa mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Manispaa ya Shinyanga na Miji inayokuwa kwa kasi ikiwemo Tinde, Didia na Iselamagazi huku ikitajwa takribani Bilioni 231 zinatarajiwa kutumika katika mradi huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa SHUWASA Mha.Yusuph Katopola amekili kupokea malekezo na ushauri wa RC Macha huku akiongeza kwa kusema kuwa Magari hayo yanakwenda kuchechemua usimamizi, ufuatiliaji na ufanisi wa mradi na lengo likiwa ni kuhakikisha huduma ya maji inafikia 95% kwa Mjini na 85% kwa Vijijini na zaidi kufikia 98% baada ya kukamilika kwa mradi huo mwaka 2028.
@wizarayamajitz
@shuwasa_on_insta
@shinyangamanispaa
@shinyangadc_official
#shinyanga_rs
No comments:
Post a Comment