MWANAMKE AKIMBILIA HOSPITALI BAADA YA KUISHI NA UJAUZITO KWA MIAKA MINNE, KIUMBE KILICHOKUWA TUMBONI KIMEFARIKI DUNIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 7 April 2025

MWANAMKE AKIMBILIA HOSPITALI BAADA YA KUISHI NA UJAUZITO KWA MIAKA MINNE, KIUMBE KILICHOKUWA TUMBONI KIMEFARIKI DUNIA


NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL KAHAMA


Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Sofia Mayega mwenye umri wa miaka 55 kutoka Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, amebainika kuishi na ujauzito kwa zaidi ya miaka minne.


Tukio hili limetokea baada ya mwanamke huyo kugundua kuwa alishindwa kujua kuwa alikuwa na ujauzito kwa kipindi chote hicho, jambo lililosababisha aishi na hali hiyo kwa muda mrefu kabla ya kutafuta msaada wa matibabu.


Sofia ameeleza kuwa alipata ujauzito akiwa na miaka 51 lakini alishindwa kugundua hali hiyo kutokana na dalili hafifu ambazo aliishi nazo kwa muda mrefu,alijua kuwa hali yake ilikuwa ya kawaida, na alijikuta akitafuta msaada kwa waganga wa kienyeji akiamini kuwa matatizo aliyokuwa nayo ni ya kawaida.


Hali hiyo ilibadilika baada ya mganga wake kufariki na kukosa huduma hali iliyopelekea mwanamke huyo kuhisi kuwa hali yake inaendelea kuwa mbaya na alipelekwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.


Huko alielekezwa kwa daktari bingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Augustino Maufi, ambaye alifanya uchunguzi wa kina na kugundua kuwa alikuwa na mimba iliyotunga nje ya mfuko wa uzazi, Hali hii ni hatari na inaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya mama kama isipopatiwa matibabu kwa wakati.


Dkt. Maufi ameeleza kuwa mimba hiyo inaweza kusababishwa na maambukizi katika mfumo wa uzazi na kwamba kama mama huyo angefika hospitalini mapema, ingaliweza kuepukika huku akiongeza kuwa hali hiyo ilimwathiri mama kwa muda mrefu na kuweza kuathiri afya yake kwa kiasi kikubwa, Hivyo, amesisitiza umuhimu wa wanawake kutembelea vituo vya afya mara kwa mara wakati wa ujauzito ili kupata huduma za afya bora.


Diwani wa kata ya Ushetu, Pili Sonje, amekiri kutokuwa na taarifa za tukio hili lakini amesisitiza umuhimu wa wanawake kuepuka kutegemea waganga wa kienyeji wakati wa ujauzito huku akiongeza kuwa ni muhimu kwa wanawake kutafuta msaada katika vituo vya afya ili kuepuka madhara kama haya na kupokea matibabu bora kutoka kwa wataalamu wa afya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso