Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Aprili 2, 2025 Kibaha mkoani Pwani katika viwanja vya Shirika la Elimu ameshiriki katika sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani humo.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.
Sherehe hizo zilizoongozwa na kauli mbiu: “ Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu” zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
Viongozi wengine ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Zungu, Rais Mstaafu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Mwisho
No comments:
Post a Comment