DC. MBONI MHITA NA WATAALAM KUTOKA WILAYA YA KAHAMA WATEMBELEA NA KUJIFUNZA MAMLAKA YA MAENEO MAALUM YA UWEKEZAJI (EPZA) - DAR ES SALAAM. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 16 April 2025

DC. MBONI MHITA NA WATAALAM KUTOKA WILAYA YA KAHAMA WATEMBELEA NA KUJIFUNZA MAMLAKA YA MAENEO MAALUM YA UWEKEZAJI (EPZA) - DAR ES SALAAM.



📌Wilaya ya Kahama katika harakati za Uwekezaji.




📍Dar es salaam.




Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Mboni Mhita pamoja na Timu ya Wataalamu kutoka Wilaya ya Kahama Aprili15, 2025 walitembelea Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji (EPZA) Jijini Dar es salaam kwa lengo la kujifunza namna ya kuendesha Maeneo Maalum ya Kiuchumi (Special Economic Zone) ambapo pamoja na mambo mengine, EPZA na Wilaya ya Kahama wamejadili namna ya kufanya ushirikiano wa karibu kwa muktadha mpana wa Wilaya ya Kahama na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.




Hatua hii imefikiwa baada ya Wilaya kuandaa Maeneo ya Uwekezaji ikiwemo Eneo Maalum la Kiuchumi la Nyanshimbi na Buzwagi, ambapo maeneo hayo tayari yana miundombinu ya msingi na baadhi ya kampuni zimeanza kuwekeza huku DC. Mnoni akibainisha baadhi ya manufaa yatakayopatikana kupitia eneo hilo la kiuchumi kuwa ni pamoja na kuharakisha usajili wa viwanda, usindikaji wa malighafi za ndani, ajira kwa wakazi wa Kahama pamoja na masoko ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa eneo hilo.




Akiwasilisha mada, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma kutoka EPZA, Bw. Panduka Yonazi alisema kuwa Wilaya imekuwa mfano wa kuigwa katika suala la harakati za kusaidia Taifa kufikia uchumi wa viwanda. Bw. Yonazi aliongeza kuwa hakuna viwanda bila maeneo ya uwekezaji, hivyo mkakati wa Wilaya katika kuandaa maeneo hayo ni sahihi kwani maeneo ya uwekezaji yamekuwa adimu katika maeneo mengi duniani. Alihimiza wilaya nyingine kuiga hatua za kiuchumi zilizochukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso