MABINTI 787 WAMEPATA VIFAA KAZI KUPITIA MRADI WA CHAGUO LANGU HAKI YANGU UNAOTEKELEZWA NA WiLDAF - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 11 March 2025

MABINTI 787 WAMEPATA VIFAA KAZI KUPITIA MRADI WA CHAGUO LANGU HAKI YANGU UNAOTEKELEZWA NA WiLDAF

 

Katibu tawala wa Wilaya Kahama Glory Absalum akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa kazi kwa mabinti waliofadhiliwa na shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF), kupitia mradi wa haki yangu chaguo langu


NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL KAHAMA

Wasichana na wanawake vijana 787 kutoka Wilaya ya Kishapu, Tarime, Butiama na Kahama wamepewa vifaa kazi kupitia mradi wa CHAGUO LANGU HAKI YANGU ambapo Vifaa hivyo vimekabidhiwa rasmi tarehe 10 Machi 2025, katika Manispaa ya Kahama  kwa lengo la kuwawezesha mabinti hao kiuchumi.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF), Aneth Mushi amesema kuwa, kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, wameweza kutambua mabinti waliosomea fani mbalimbali kama vile Ushonaji, Ususi, Mapambo, Ufundi Umeme, Magari, Bomba, Mapishi, Ukarani na Uchomeleaji na Vifaa hivyo vimekabidhiwa kulingana na fani walizosomea ili kuwasaidia katika kujiendeleza kiuchumi.


Mgeni Rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Glory Absalum, amewashauri wazazi wa mabinti hao kuwa nyuma yao ili vifaa hivyo vikafanye kazi iliyokusudiwa na kuvitunza kama sehemu ya kukuza uchumi wa familia zao, badala ya kuviweka kama dhamana katika mikopo.


Pia amewahimiza mabinti hao kutumia vifaa hivyo kwa manufaa yao na kufanya kazi kwa bidii ili waweze kupata mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri.


Mmoja wa mabinti waliopokea vifaa, Elizabeth Alex, amewashukuru WiLDAF kwa kuwawezesha kupata ujuzi na vifaa, na kuomba mashirika mengine kuunga mkono jitihada za kuwapa fursa mabinti wengine.


Afisa Ustawi wa Jamii, Swahiba Chemchem, ameeleza kuwa mradi wa CHAGUO LANGU HAKI YANGU unalenga kuboresha mifumo ya huduma salama za afya ya uzazi na kuzuia ukatili wa kijinsia, hasa kwa mabinti balehe na wanawake vijana, wakiwemo wenye ulemavu.


Mradi huu pia unalenga kuwapatia ujuzi mabinti ili waweze kujikwamua kiuchumi na kujilinda dhidi ya vitendo vya kikatili na ndoa za utotoni.


Kwa ujumla, mradi umefanikiwa kutoa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 49 kwa mabinti 281 wa Wilaya ya Kahama, huku gharama zote za ufadhili zikifikia zaidi ya shilingi bilioni 34.


Katibu tawala wa Wilaya Kahama Glory Absalum akikabidhi vifaa kazi kwa mabinti waliofadhiliwa na shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF), kupitia mradi wa haki yangu chaguo langu

Katibu tawala wa Wilaya Kahama Glory Absalum akikabidhi vifaa kazi kwa mabinti waliofadhiliwa na shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF), kupitia mradi wa haki yangu chaguo langu

Katibu tawala wa Wilaya Kahama Glory Absalum akikabidhi vifaa cheti cha shukrani kwa  shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF)
Mmoja wa mabinti waliopokea vifaa, Elizabeth Alex, akiwashukuru WiLDAF kwa kuwawezesha kupata ujuzi na vifaa, na kuomba mashirika mengine kuunga mkono jitihada za kuwapa fursa mabinti wengine.
Mmoja wa wazazi aliyehudhuria akiwashukuru WiLDAF kwa kuwawezesha watoto wao kupata ujuzi na vifaa, 
kwa niamba ya wazazi wenzake
Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa kwa mabinti kupitia mradi wa haki yangu chaguo langu
Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa kwa mabinti kupitia mradi wa haki yangu chaguo langu
Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa kwa mabinti kupitia mradi wa haki yangu chaguo langu
Afisa Ustawi wa Jamii, Swahiba Chemchem, akisoma mradi wa CHAGUO LANGU HAKI YANGU unalenga kuboresha mifumo ya huduma salama za afya ya uzazi na kuzuia ukatili wa kijinsia, hasa kwa mabinti balehe na wanawake vijana, wakiwemo wenye ulemavu.
Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa kwa mabinti kupitia mradi wa haki yangu chaguo langu
Baadhi ya mabinti wakiimba na kucheza 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso