WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA KUZAMA KATIKA SHIMO LA MAJI LENYE KEMIKALI ZA DHAHABU SIMIYU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 28 March 2025

WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA KUZAMA KATIKA SHIMO LA MAJI LENYE KEMIKALI ZA DHAHABU SIMIYU


Na Belens China, Simiyu


Watoto wawili wa familia moja katika kijiji cha Bulumbaka, kata ya Mwaubingi, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, wamefariki dunia baada ya kudumbukia katika shimo la maji yanayosadikiwa kuwa na kemikali za kuchenjua dhahabu kutoka mgodi wa Gasuma Namba Moja ulipo katika kijiji hicho.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Simiyu, ASF Faustin Mtitu, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo cha vifo vya watoto hao ni kunywa maji hayo yenye kemikali na kukosa hewa ya oksijeni.

Watoto hao, Yona Chai mwenye umri wa miaka 7 na Baraka Balida mwenye miaka 3, walikutwa wakiwa kwenye shimo hilo.

Tukio hili linatoa wito kwa jamii kuwa makini na mazingira yenye hatari, hasa katika maeneo yanayohusiana na shughuli za uchimbaji madini.

Mwisho.






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso