NA NEEMA NKUMBI- HUHESO DIGITAL KAHAMA
Wananchi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wamehimizwa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wanaopata ajali, wajawazito, na watoto wachanga wanaohitaji huduma ya haraka katika hospitali.
Hayo wamesemwa march 7, 2025 na Mratibu wa Damu Salama Hospitali ya Manispaa ya Kahama Noel Malaki, akisisitiza umuhimu wa zoezi la kuchangia damu, na akatoa takwimu za matumizi ya damu, akisema kila siku hutumika chupa 10-20 na kwa mwezi hutumika chupa 450-600.
Noel amesema "Hospitali ya Manispaa ya Kahama inatumia wastani wa chupa 400 hadi 600 za damu kila mwezi, na damu inayopatikana hutumika katika vituo vyote vya kutolea huduma katika Wilaya ya Kahama na nje ya wilaya".
Derick Massy, mdau wa sekta ya afya amesema zoezi hilo linachangia kwa kiasi kikubwa kutoa huduma ya haraka kwa wagonjwa, hasa wale wanaohitaji damu kutokana na ajali au magonjwa ya dharura huku akiwahimiza wananchi kuchangia damu ili kusaidia jamii kwa ujumla.
Baraka Moshi Majengo, Mwenyekiti wa CHAMAUKA, amewahimiza waendesha bodaboda na wauza matunda kujitokeza na kusaidia watu, huku akisisitiza umuhimu wa kusaidia wagonjwa.
Mafundi Ujenzi waliojitokeza kuchangia damu, kama Leonard Kamata amesema wamewiwa kuchangia damu kwa sababu hosipitali ina mahitaji mengi hasa wajawazito, wangonjwa wanaofanyiwa upasuaji na watoto.
Samson Shamba amesema damu waliochangia itawasaidia akinamama wajawazito na watu wanaopata ajali.
Leo, chupa 29 za damu zimekusanywa kutoka kwa chama cha Mafundi Ujenzi Kahama (CHAMAUKA).
No comments:
Post a Comment