RC MACHA AMEWATAKA WAFANYABIASHARA NA WANANCHI KUTOA NA KUDAI RISITI HALALI. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 1 March 2025

RC MACHA AMEWATAKA WAFANYABIASHARA NA WANANCHI KUTOA NA KUDAI RISITI HALALI.

Mkuu wa Mkoa Shinyanga Anamringi Macha (Kushoto) akikabidhi tuzo kwa walipakodi wakubwa Mkoa ashinyanga na Mkoa wa kikodi Kahama.
Mkuu wa Mkoa Shinyinga Anamringi Macha aliyevaa tai ya rangi ya kijivu na suti, kushoto ni Mkuu wa Wilaya Kahama aliyevaa gauni refu lenye maua ya njano na viongozi wengi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara Mkoa wa Shinyanga.


NA NEEMA NKUMBI- HUHESO DIGITAL KAHAMA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amewataka Wafanya biashara na wananchi wa Mkoa wa shinyanga kutoa na kudai risiti halali na kutunza risiti hizo kwani inawajengea wananchi kuwa na uhalali wa vitu walivyonunua.

Akizungumza februari 28, 2025 katika hafla ya Tuzo kwa walipa kodi 2023/2024, Mkoa wa Kikodi Kahama, Rc Macha amesema ulipaji kodi sio shuruti ni maamuzi hivyo wafanyabiashara watozwe kodi kulingana na biashara zao wasitozwe zaidi wala kupungua.


Rc Macha amesema, " Lazima tuwe wazalendo kwa kulipa kodi ili TRA waweze kufika Malengo kwani wasipofika malengo huwa nawaita na kuwauliza kwa nini hawajafika malengo pia wakifanya zaidi huwa nawaita ili kujua wamefanyaje ili kuvuka lengo, hivyo TRA msiwatoze zaidi wafanyabiashara kwa lengo la kuvuka malengo na wafanyabiashara waendelee kujitoa kwa hiari kulipa kodi".


Rc Macha amekemea uingizwaji wa bidhaa za nje kwa magendo zinasababisha nchi kukosa mapato pia zinadidimiza biashara hapa nchini kwani zinaingizwa kwa bei ndogo na wafanyabiashara wanashindwa kuuza bidhaa zinazotoka hapa nchini.


Pia amesisitiza kuwa na mawasiliano ya karibu na TRA, pia watoe taarifa TRA pale wanapotaka kubadilisha biashara ili waweze kulipa kodi sawasawa na biashara wanazofanya na kuwa mabalozi kwa wafanya biashara wengine katika suala la uzalendo katika kulipa kodi.

Akisoma Hotuba ya TRA Emanuel Nnko amesema wamejidhatiti kuhakikisha wanaongeza ubora wa huduma zinazozingatia weledi, uwajibikaji na uadilifu ili kufanikisha ukusanyaji wa mapato unaongezeka.

"Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 TRA Mkoa wa shinyanga na Mkoa wa kikodi Kahama Tumefanikiwa kukusanya zaidi ya bilion 34 ikiwa ni sawa na asilimia 132.05% ya lengo la kiasi cha shilingi bilion 25.777 iliyopangiwa kukusanya kwa mwaka husika", amesema Emanuel.

Emanuel ameongeza kuwa katika kipindi cha mwezi julai 2024 hadi januari 2025 Mkoa wa Shinyanga na Mkoa wa kikodi Kahama wamefanikiwa kukusana zaidi ya bilion 36 sawa na ufanisi wa asilimia 114.03% ya lengo la kukusanya shilingi bilion 32.25.

Emanuel ameeleeza kuwa kuna baadhi ya wafanya biashara wanaendesha biashara zao bila kusajiliwa na mamlaka ya mapato yaani kupatiwa namba ya mlipakodi (TIN) na wengine kutumia TIN ambazo si za matumizi ya biashara jambo ambalo husababisha upotevu wa mapato ya serikali.

Emanuel amefafanua kwamba kwakutambua umuhimu wa walipakodi, serikali kupitia mamlaka ya mapato imeandaa siku ya shukrani kwa mlipakodi kwa ajili ya kuwatambua na kuwashukuru kwa mchango wao kwa taifa pia kuwatunuku vyeti na zawadi ili kuwatia moyo na kuwapa hamasa wengine kufanya vizuri zaidi.

TRA Mkoa wa Shinyanga na Mkoa wa kikodi Kahama imewatambua taasisi zenye ushirikiano mzuri katika kukusanya kodi, walipakodi bora wa Mkoa na Wilaya, walipakodi wadogo wa Mkoa, walipakodi wa Kati Mkoa, walipakodi wakubwa wa Mkoa, walipakodi wakubwa wa Mkoa na wachangiaji wakubwa wa Mkoa, walipakodi kutoka idara ya walipakodi wa kati na walipakodi kutoka idara ya walipako wakubwa.

Awali akitoa salamu za Wilaya ya Kahama, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita amesema wafanyabiashara wamekuwa mstari wa mbele kuomba kupata EFD mashine kwa ajili ya kulipa kodi hali hii inaenda kuchochea ulipaji wa kodi na ni chachu ya maendeleo ndani ya nchi yetu.


Kauli mbiu ya Mamlaka ya mapato Tanzania TRA ni " PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU".
Mkuu wa Mkoa Shinyanga Anamringi Macha (Kushoto) akikabidhi tuzo kwa walipakodi wakubwa Mkoa ashinyanga na Mkoa wa kikodi Kahama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita akikumbatiana kwa furaha na Katibu tawala wa Wilaya ya Kahama baada ya kupewa cheti cha Taasisi yenye ushirikiano Mzuri katika kukusanya kodi.
Katibu Tawala Wilaya ya Kahama (Kushoto) akikabidhi cheti kwa walipakodi wakubwa Mkoa ashinyanga na Mkoa wa kikodi Kahama.

Mkuu wa Mkoa Shinyanga Anamringi Macha (Kushoto) akikabidhi tuzo kwa walipakodi wakubwa Mkoa ashinyanga na Mkoa wa kikodi Kahama.
Katibu Tawala Wilaya ya Kahama (Kushoto) akikabidhi cheti kwa walipakodi wakubwa Mkoa ashinyanga na Mkoa wa kikodi Kahama.

Mkuu wa Mkoa Shinyanga Anamringi Macha (Kushoto) akikabidhi cheti kwa walipakodi wakubwa Mkoa ashinyanga na Mkoa wa kikodi Kahama..
Mkuu wa Mkoa Shinyinga Anamringi Macha aliyevaa tai ya rangi ya kijivu na suti, kushoto ni Mkuu wa Wilaya Kahama aliyevaa gauni refu lenye maua ya njano na viongozi wengi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa Shinyanga Anamringi Macha (Kushoto) akikabidhi cheti kwa walipakodi wakubwa Mkoa ashinyanga na Mkoa wa kikodi Kahama

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso