Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha Akabidhi Zawadi kwa Watoto Yatima na Waliotelekezwa kwa Niaba ya Rais Samia kwa ajili ya sikukuu ya eid al-fitr.
NA NEEMA NKUMBI -HUHESO DIGITAL KAHAMA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, amekabidhi zawadi kwa vituo vinne vya kulelea watoto yatima, waliotelekezwa, na watoto wanaotoka katika mazingira magumu katika Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga, kwa ajili ya sherehe za Sikukuu ya Eid al-Fitr.
Vituo hivyo ni Mvuma Ophanage center, Kahama peace Ophanage center, Zakana Ophanage center, New Hope Ophanage center vilivyopo Manispaa ya Kahama, Shinyanga Society for Ophance, Makazi ya wazee Kolandoto vituo hivi vinapatikana Manispaa ya Shinyanga na Kishapu Mwadui Home Kilichopo Kishapu.
Zawadi hizo ni sehemu ya msaada kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni ishara ya mshikamano na upendo kwa watoto wa familia zisizo na uwezo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mhe. Macha amesisitiza kuwa kutelekeza watoto ni dhambi kubwa na amewataka wazazi kuwajibika katika kulea watoto wao, akikemea tabia ya baadhi ya wazazi kupeleka watoto kwa mabibi zao na kuwaacha, akisema kuwa hali hiyo inawaathiri watoto na ni unyanyasaji kwa wazee ambao wanahitaji uangalizi wao.
RC Macha Amewataka wabibi kutoa taarifa kwa viongozi wa vijiji kuhusu hali ya kutelekezwa kwa watoto ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
"Tunaona watoto wanatelekezwa, mtoto anazaliwa mama anamuacha, kama hauwezi kulea bora ukamleta mtoto ustawi wa jamii ukaeleza sababu za kushindwa kulea mtoto, Ni dhambi kubwa kumtekelekeza mtoto na nyie akina bibi acheni kupokea watoto wa mabinti zenu, kila mzazi atunze mtoto wake," amesema Mhe. Macha.
Pia, Mhe. Macha amesisitiza kuwa ni utamaduni wa Watanzania kushirikiana na kusaidiana katika kipindi cha sikukuu na kusema kuwa Rais Samia ameona kuwa kuna watoto ambao hawana uwezo wa kusherehekea kama wenzao, na kwa hiyo ameamua kutoa msaada ili kila mtoto asherehekee na kufurahi, huku akiwahakikishia kuwa watoto wote waliopo katika vituo maalum kuwa wao ni watoto wa Rais Samia na wanapendwa.
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kahama, Bi. Swahiba Chemchem, amesema kuwa vituo hivyo vinahifadhi watoto yatima, waliotelekezwa, na watoto wa kigeni kutoka nje ya nchi ambao wamekuja nchini kwa ajili ya kazi na kusema kuwa Kituo cha New Hope Orphanage kinahifadhi watoto wa kigeni kwa muda hadi utaratibu wa kuwawezesha kurudi kwao utakapo kamilika.
Mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha New Hope Orphanage kilichopo Mtaa wa Mwime, Kata ya Zongomela, Arnold Zakaria (15) kutoka Burundi, ametoa shukrani kwa Rais Samia kwa msaada huo na kusema kuwa wamefurahi na wanamuombea kwa Mungu abarikiwe.
Watoto, wasimamizi, na wamiliki wa vituo hivyo wametoa shukrani kwa Rais Samia kwa msaada huo na wameahidi kumuombea kwa Mungu, wakimtaka akumbuke na watoto wengine ambao wako mitaani bila uangalizi.
Katika mkoa wa Shinyanga, jumla ya watoto zaidi ya 300 wametembelewa katika vituo saba, vikiwemo viwili kutoka Shinyanga Manispaa, kimoja kutoka Kishapu, na vinne kutoka Manispaa ya Kahama, Vituo hivyo vimepokea msaada wa zaidi ya kilo 800 za mchele, mafuta ya kupikia lita 300, sukari kilo 400, sabuni ya unga mifuko 18, mbuzi zaidi ya 14, juisi, pamoja na maji.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha Akabidhi Zawadi kwa Watoto Yatima na Waliotelekezwa kwa Niaba ya Rais Samia kwa ajili ya sikukuu ya eid al-fitr.

Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kahama, Bi. Swahiba Chemchem akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kutoka kwa Rais Samia

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha Akabidhi Zawadi kwa Watoto Yatima na Waliotelekezwa kwa Niaba ya Rais Samia kwa ajili ya sikukuu ya eid al-fitr.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha Akabidhi Zawadi kwa Watoto Yatima na Waliotelekezwa kwa Niaba ya Rais Samia kwa ajili ya sikukuu ya eid al-fitr.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha Akabidhi Zawadi kwa Watoto Yatima na Waliotelekezwa kwa Niaba ya Rais Samia kwa ajili ya sikukuu ya eid al-fitr.

Mkuu wa Mkoa Wa Shinyanga Anamringi Macha akipika wali katika kituo cha kulea watoto cha Mvuma kilichopo Mtaa wa Nyakato Kata ya Nyasubi.

Mkuu wa Mkoa Wa Shinyanga Anamringi Macha na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita wakikata nyama katika kituo cha kulea watoto cha Mvuma kilichopo Mtaa wa Nyakato Kata ya Nyasubi.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita akipika wali katika kituo cha kulea watoto cha Mvuma kilichopo Mtaa wa Nyakato Kata ya Nyasubi.

Mkuu wa Mkoa Wa Shinyanga Anamringi Macha na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita wakikata nyama katika kituo cha kulea watoto cha Mvuma kilichopo Mtaa wa Nyakato Kata ya Nyasubi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha Akabidhi Zawadi kwa Watoto Yatima na Waliotelekezwa kwa Niaba ya Rais Samia kwa ajili ya sikukuu ya eid al-fitr.

No comments:
Post a Comment