RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA MISRI, MHE. BADRABDELATTY, ZANZIBAR - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 20 March 2025

RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA MISRI, MHE. BADRABDELATTY, ZANZIBAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Machi 20, 2025 amekutana na kuzungumza na Mjumbe Maalum wa Rais wa Misri, Mhe. Badr Abdelatty ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri Waishio Nje wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Ikulu ndogo ya Tunguu - Zanzibar.


Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Naibu Katibu Mkuu Nishati - Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio pamoja na Viongozi wengine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso