HALMASHAURI YA USHETU YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI BILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIKOPO YA ASILIMIA10 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 7 March 2025

HALMASHAURI YA USHETU YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI BILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIKOPO YA ASILIMIA10




NA NEEMA NKUMBI-HUHESO DIGITAL MSALALA


Halmashauri ya Ushetu imekabidhi hundi ya shilingi bilion 1.3 kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na kila Halmashauri nchini.


Akizungumza na waandishi wa habari march 6, 2025 katika maadhimisho ya siku ya wanawake Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika Bugarama Halmashauri ya Msalala, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Hadija Kabojela amesema fedha hizo zimetokana na mapato ya ndani ya asilimia 10%.


Hadija amefafanua kuwa kati ya fedha hizo milion 500 ni kwa ajili ya wanawake, milion 300 vijana na milion 100 ni kwa ajili ya wenye ulemavu.


Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Rehema Edson, amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Mkoa wa Shinyanga umepanga kutoa zaidi ya shilingi bilioni 5, na hadi kufikia Februari 2025, zimetolewa zaidi ya shilingi bilioni 2 kwa vikundi 119 vya wanawake, 110 vya vijana, na vikundi 10 vya watu wenye ulemavu.


Aidha MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewasihi wanawake na wasichana mkoani Shinyanga kujitokeza kwa wingi kushiriki katika fursa mbalimbali za kiuchumi na ujasiriamali zinazojitokeza ili kujiimarisha kiuchumi.





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso