HALMASHAURI YA MSALALA IMETENGA MILIONI 400 KWA AJILI YA KUTATUA CHANGAMOTO YA MADAWATI KATIKA SHULE ZA MSINGI. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 1 March 2025

HALMASHAURI YA MSALALA IMETENGA MILIONI 400 KWA AJILI YA KUTATUA CHANGAMOTO YA MADAWATI KATIKA SHULE ZA MSINGI.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Msalala

NA NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL MSALALA


Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa Shinyanga Anamtingi Macha aliwasisitiza wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha wanatekeleza agizo la serikali kuwa wanafunzi wanakaa katika madawati.


Wakizungumza katika baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Msalala februari 28, 2025, Diwani wa kata ya Mwalugulu Flora Sagasaga alitaka ufafanuzi juu ya upungufu wa madawati katika baadhi ya shule za msingi huku wanafunzi wakiendelea kukaa chini.


Naye Diwani wa kata ya Ikinda Matrida Msoma naye aliibua hoja ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya matundu ya vyoo huku akitaka ufafanuzi juu ya uhamisho wa makaburi yaliyoko katika eneo la shule na nini kifanyike kuondoa changamoto hiyo.


Akijibu maswali ya madiwani hao Mwenyekiti wa kamati ya elimu ambaye ni diwani wa kata ya Segese Joseph Manyala amesema wametenga zaidi ya shilingi milioni 400 kwa ajili ya ukarabati na utengenezaji wa madawati ambapo mpaka sasa madawati 400 yameshaanza kutengenizwa na yakikamilika yapelekwa katika shule ambazo zinauhitaji zaidi.


"Tumwyoa maelekezo kwamba madawati ambayo yatakuwa yamekamilika yapelekwe kwenye shule ambazo zinauhitaji zaidi hivyo kufikia april 20, 2025 kati itakuwa imekamilika", amejibu Joseph.


Pia amesema kuhusu suala la Makaburi tayari wenye makaburi hayo wameahalipwa fidia hivyo baada ya miezi miwili makaburi hayo yatakuwa yameshahamishwa, pia ameeleza kuwa fedha zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi waatundu ya vyoo ziko ndani ya uwezo wao.


Akitoa salamu za Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita amewataka madiwani hao kuwa na kauli moja na kushirikiana katika kuleta maendeleo katika jimbo lao pia amewaasa TFS kushirikiana taasisi zingine pale wanapofanya opareshani zao.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso