Na. Paul Kasembo, KAHAMA DC.
Mkuu wa Walaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita leo Machi 27, 2025 amemkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndg. Stephen Masato Wasira katika ziara yake ya Chama wilayani Kahama ambapo pamoja na mambo mengine ndugu Wasira atafanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika viwanja vya Stendi ya mabasi madogo (CDT), Manispaa ya Kahama.
Hii ni siku ya pili ya ziara ya ndugu Wasira ambapo kesho Machi 28, 2025 atahitimisha ziara yake ya siku tatu katika Wilaya ya Kishapu.
@ortamisemi
@ccmtanzania
@mboni_mhita
@kishapudc
@kahamamc_official
#shinyanga_rs
No comments:
Post a Comment