HALMASHAURI YA MANISPAA YA KAHAMA KWA KUSHIRIKIANA NA RAILWAY CHILDREN AFRICA WAMEZINDUA MRADI WA KUHUDUMIA WATOTO WANAOISHI NA KUFANYA KAZI MTAANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 14 February 2025

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KAHAMA KWA KUSHIRIKIANA NA RAILWAY CHILDREN AFRICA WAMEZINDUA MRADI WA KUHUDUMIA WATOTO WANAOISHI NA KUFANYA KAZI MTAANI




Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa Kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la "Railway Children Africa" wamezindua Mradi wa kuhudumia Watoto wanaoishi na kufanya Kazi mitaani hususan Maeneo ya Stendi.


Moja kati ya Mkakati wa Kufanikisha mradi huo ni pamoja na kuanzisha Madawati ya kusimamia ulinzi na usalama wa Watoto wanaopatikana Maeneo ya Stendi.


Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Ndg. Baraka Msumi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo wakati wa Kikao cha Pamoja cha Uzinduzi wa Mradi huo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama. 


Akifungua kikao hicho Ndg. Tumshukuru Mudui kwa niaba ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama amesema kuanzishwa kwa Mpango huo utaenda kusaidia kubaini na kutambua changamoto za watoto zinazopelekea kukimbia huko watokako na kuzipatia ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso