Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amekutana na kujadiliana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, kuhusu juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa haya mawili kwenye sekta ya afya.
Majadiliano hayo yaliyofanyika leo, Januari 14, 2025 jijini Dodoma, Mhe. Dkt. Molel akimuwakilisha Waziri wa Afya Mhe, Jenista Mhagama, yamejikita katika kuboresha huduma za afya, hasa kwenye mapambano dhidi ya Kifua Kikuu (TB), malaria na UKIMWI.
Aidha, yamegusia suala la Bima ya Afya kwa wote (Universal Health Insurance), huduma za afya za mama na mtoto pamoja na kujadili mbinu za kupunguza vifo vya wajawazito na vifo vya watoto wachanga.
Katika majadiliano hayo, Norway imeonyesha nia ya kuchangia maboresho ya sekta ya afya kupitia ushirikiano wa kimataifa, huku viongozi hao wakiahidi kuimarisha uhusiano wa muda mrefu baina ya Tanzania na Norway ili kufanikisha afua za afya zinazolenga kuboresha ustawi wa wananchi.
No comments:
Post a Comment