ZAIDI YA WATOTO ELFU 36 WANAISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU-KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 6 December 2024

ZAIDI YA WATOTO ELFU 36 WANAISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU-KAHAMA





NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL KAHAMA

Zaidi ya watoto elfu 36 wanaishi katika mazingira magumu katika Manispaa ya Kahama hii imetokana na takwimu za mwezi novemba 2024 zilizotolewa na Manispaa ya kahama.


Akizungumza leo desemba 6, 2024 katika maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama amesema kuna changamoto ya watoto wanaoishi mtaani hali unayosababishwa na matokeo ya ukatili.


Kwela amesema, " zaidi ya watoto elfu 36 wanaishi mitaani, shida moja kubwa tunapokea watoto kutoka nje ya nchi na mikoa jirani, inawezekana sababu ya mazingira mazuri na uchangamfu wa biashara, ajira kwa watoto wazazi kuachana inawezeka hii ndio imekuwa chachu ya kuwavuta watoto kuwa wengi mtaani".


Afisa Uhamiaji Wilaya ya Kahama Salum Rashid amesema kuna Utumikishwaji mkubwa wa watoto kutoka nje ya nchi hivyo kuwatumikisha watoto walio chini ya miaka 18 ni kosa kisheria kwani watoto wengi wanakuwa wahanga wa vitendo vya kikatili kama kupigwa na kubakwa.


Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kishimba Susan Elia ameiomba serikali kutia nguvu katika ulinzi zidi ya ukatili kwani wanapata hofu wakiwa wanatembea kwenda na kutoka shuleni kuwa wanaweza wakafanyiwa ukatili wa kingono wakiwa njiani.


Akitoa maelekezo ya Serikali Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama Hamad Mbega, amesema jeshi la polisi, mahakama, hospitali na ustawi wa jamii kutoa kipaumbele katika kushughulikia maswala ya ukatili kwa kuweka vikao vya kutathimini mienendo ya utoaji huduma kwa wahanga wa ukatili.


Mbega amesema Mahakama zisipindishe sheria kwa wahusika wa vitendo vya ukatili wachukuliwe hatua kwa haraka kwa kufanya hivyo kutawapa moyo wananchi wanaotoa taarifa juu ya ukatili pia watoto mashuleni wapewe ulinzi kwa kupewa walimu watakao wasimamia na kutoa taarifa wanapopatwa na changamoto ya ukatili.

Mbega amewaonya wanaowaodhesha watoto waliochini ya miaka 18 kuwa nikosa kisheria hivyo atakayeshiriki katika kuodhesha watoto atachukuliwa hatua kali za kisheria.


Awali akisoma historia ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amesema kampeni hii ni ya kimataifa iliyoanzishwa tangu mwaka 1991.


Kauli mbiu ya mwaka huu ni "MIAKA 30 YA BEIJING CHAGUA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA".



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso