NA NEEMA NKUMBI -HUHESO DIGITAL KAHAMA
Wenyeviti wa Serikali za mitaa Kata ya Mhongolo wamekabidhiwa mihuri na hati za kiapo walizosaini leo desemba 03, 2024 tayari kwa kuanza kazi rasmi.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Afisa Mtendaji wa Kata ya Mhongolo Boniphace Maziku amesema viongozi wa mitaa waliochanguliwa, wahakikishe wanafuata taratibu na kuitisha mikutano ya hadhara pia kuwasomea wananchi mapato na matumizi.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Kata ya Mhongolo Juliana Bruno amewaasa viongozi hao kutenda haki pia kushirikiana na vyama pinzani katika kuleta maendeleo kwani uchaguzi umepita na sasa ni wamoja.
Naye mwenyekiti wa Mtaa wa Mhongolo Emanuel Nangale amesema wamejipanga vyema kwenda kutekeleza majukumu yao, poa kusoma mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu.
Nangale ameeleza kipaumbele chake kuwa ni elimu kwa kuanzisha shule ya sekondari kwa kidato cha tano na cha sita pia akiweka kipaumbele katika miundo mbinu ya barabara, umeme na maji.
Aidha Mwenyekiti wa serikali za mtaa wa Mbulu Mision Solomoni Ruta amesema mtaa huo unachangamoto ya kutokuwa na shule ya sekondari watoto wamekuwa wakitembea kwa umbali mrefu ili kurudisha tumaini kwa wananchi na watoto wao kipaumbele chao itakuwa ni ujenzi wa shule hiyo.
No comments:
Post a Comment