NAZIELEKEZA HALMASHAURI ZOTE SITA MKOANI SHINYANGA KUTOA FEDHA ZA LISHE KWA WAKATI - RAS CP. HAMDUNI. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 19 December 2024

NAZIELEKEZA HALMASHAURI ZOTE SITA MKOANI SHINYANGA KUTOA FEDHA ZA LISHE KWA WAKATI - RAS CP. HAMDUNI.



Na. Paul Kasembo, SHY RS.

KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni amezielekeza Halmashaufi zote 6 za Mkoa wa Shinyanga kupitia Waganga Wakuu kuhakikisha kuwa fedha zote za utekelezaji wa shughuli za lishe zilizotengwa zinatolewa kwa wakati na kuendelea kusimamia utekelezaji wa mkataba wa lishe ikiwemo utoaji wa chakula shuleni.


RAS CP. Hamduni ameyasema haya leo terehe 19 Desemba, 2024 alipokuwa akifungua warsha ya kuboresha huduma za lishe kwa mama na mtoto mkoani Shinyanga ambayo imejumuisha wadau mbalimbali kutoka Wizara ya TAMISEMI, Afya, Mkoa wa Shinyanga na Tabora huku akiwaahidi washiriki kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wadau katika kuinua hali ya lishe hapa Shinyanga na kuimarisha afua za afya na uzazi.


"Nitumie nafasi hii kuzielekeza Halmashauri zote 6 za Mkoa wa Shinyanga kupitia Waganga Wakuu kuhakikisha kuwa fedha zote za utekelezaji wa shughuli za lishe zilizotengwa zinatolewa kwa wakati na kuendelea kusimamia utekelezaji wa mkataba wa lishe ikiwemo utoaji wa chakula shuleni,"amesema RAS CP. Hamduni.


Awali akitoa taswira ya warsha hii ndg. Yassin Ally ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kivulini amesema kuwa wamekutana hapa na wadau wa lishe kwa mama na mtoto hapa Shinyanga ili kujadili mikakati ya kuboresha huduma hizo na kuangalia fursa za rasilimali zilizopo ili ziweze kutumika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkataba uliowekwa kati ya Serikali na Wakuu wa Mikoa wote.


Pia kuangazia fursa zinazopatikana katika Mkoa huu na namna bora ya kuzitumia ili zilete matokeo chanya na makubwa zaidi kama Serikali inavyotarajia kwa kufuata Sera na Miongozo ya Wizara ya TAMISEMI na Afya.


Takwimu za lishe zinaonesha kuwa Udumavu kwa watoto chini ya miaka 5 umepungua kutoka asiliamia 32.1 hadi 27.5 ukondefu kutoka asilimia 4.3 hadi 1.3 na hii inaonesha kuwa juhudi zetu za kupambana na utapiamlo zinaleta matunda ijapokuwa kiwango cha udumavu bado ni kikubwa na hivyo muhimu kuendelea kusimamia utekelezaji wa afua ya lishe mkataba watika maeneo yetu.




Serikali ya Mkoa wa Shinyanga inawashukuru wadau wote wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali likiwemo Kivulini na World Vision Tanzania ambao wanafanya kazi kwa pamoja katika kutekeleza afua mbalimbali zinazolenga masuala ya lishe na afya ya mama na mtoto katika Halmashauri ya Kishapu na Shinyanga DC kupitia mradi wa GROW ENREACH na NOURISH unaotekelezwa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu pekee.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso