SERIKALI INATAMBUA, KUHESHIMU NA KUTHAMINI MCHANGO WA MADHEHEBU YA DINI LIKIWEMO KANISA KATOLIKI - RC MACHA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 19 December 2024

SERIKALI INATAMBUA, KUHESHIMU NA KUTHAMINI MCHANGO WA MADHEHEBU YA DINI LIKIWEMO KANISA KATOLIKI - RC MACHA.


Na. Paul Kasembo, SHY RS.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa Serikali inatambua, inaheshimu na kuthamini kazi na mchango mkubwa unaotolewa na madhehebu ya dini likiwemo Kanisa Katoliki huku akiwaomba waumini kuendelea kumuombea baraka Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake ili aendelee kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi wake wakiwemo wa Shinyanga.


RC Macha ameyasema haya leo tarehe 19 Desemba, 2024 wakati wa Misa ya Utolewaji wa Daraja la Ushemasi kwa Deusdedith Nkandi ambapo pamoja na mambo mengine amempongeza sana kwa hatua hii na kumuahidi kuwa Serikali inamtegemea sana na kwamba itafanya naye kazi wakati wote ili aweze kufikia malengo yake ya kwenda kuhubiri neno la Mungu na kutangaza upendo kwa msaada wa Roho Mtakatifu na kumuomba pia kwenda kuwahamasisha vijana wafanye kazi kwa bidii na waishi maisha mema yenye kumpende Mwenyezi Mungu.


"Serikali inatambua, inaheshimu na inathamini sana mchango wa madhehebu ya dini zote likiwemo Kanisa Katoliki, na kipekee kabisa nimpongeze Shemasi Nkandi na nimuahidi tu kuwa Serikali tutafanya naye kazi wakati wote na ukumbuke tu kuwa kwa kuwa wewe bado ni kijana, tunakutegemea sana kwenda kuwasaidia vijana wenzio waweze kuishi maisha mema ya kumpendeza Mungu na wafanye kazi pia kwa juhudi," amesema RC Macha.


Ibada hii ya kumpandisha daraja Shemasi Nkandi imefanyika katika Kanisa Kuu la Mama mwenye huruma lililopo Ngokolo Manispaa ya Shinyanga imeongozwa na Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akiwa na mwenyeji wake Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso