RC MACHA AKABIDHI VIFAA VYA KUJIFUNZIA KAZI ZA MIKONO KWENYE HALMASHAURI ZA SHINYANGA, - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 18 December 2024

RC MACHA AKABIDHI VIFAA VYA KUJIFUNZIA KAZI ZA MIKONO KWENYE HALMASHAURI ZA SHINYANGA,

 



Na. Paul Kasembo, Shy Rs.


MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekabidhi vifaa vya kujifunzia kazi za mikono kwenye karakana za mabinti kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze kwa niaba ya Wakurugenzi wa Halmashauri nyingine za Shinyanga, vifaa ambavyo vitafungwa kwenye karakana za mafunzo kwa vitendo za mradi wa EpiC na vitaenda kutumika katika vituo vya kutolea huduma za afya katika Halmashauri hizo.


RC Macha amekabidhi makabati ya kuhifadhia kumbukumbu za wapokea huduma, komputa, printer, vyerehani, mashine za kushonea masweta, majora ya vitaa na kifaa cha kuosha na kukausha nywele kwenye saloon venye jumla ya shilingi Milioni 63 ambavyo vitafungwa kwenye karakana za mafunzo kwa vitendo za mradi wa EpiC Mkoani Shinyanga.


Aidha vifaa hivi vimetolewa chini ya usimamizi wa mradi wa Meeting Targets and Maintaining Epindemic Control (EpiC) kwa kushirikiana na shirika la Family Health International (FHI 360) linalofadhiliwa na mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani (PEPFAR) kupitia Serikali ya wa watu wa Marekani (USAID).


Kwa Mkoa wa Shinyanga, mradi wa EpiC ulianza Machi 2020 na utaendelea mpaka Septemba 2025 na unatekelezwa katika Halmashauri tano kupitia Asasi za kiraia ya SHDEPHA+ katika Halmashauri za wilaya ya Shinyanga, Msalala na Shinyanga Manispaa pia HUHESO Foundation inatekeleza mradi katika Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Kahama Manispaa. ukiwa na malengo ya utoaji wa elimu juu ya VVU, jinsi ya kujikinga ili kuzuia maambukizi mapya, mabadiliko ya tabia hatarishi na upimaji wa VVU ngazi ya jamii. Sambamba na hilo mradi unatoa mafunzo rasmi na kazini kwa watoa huduma za afya kulingana na taratibu za Serikali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso