NAIBU WAZIRI ZAINAB KATIMBA AMESEMA HARIDHISHWI NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA BARABARA MANISPAA YA KAHAMA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 4 December 2024

NAIBU WAZIRI ZAINAB KATIMBA AMESEMA HARIDHISHWI NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA BARABARA MANISPAA YA KAHAMA.

Naibu Waziri wa Nchi, TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Ujenzi wa miundombinu wa TACTIC wilayani Kahama, kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa haraka na kwa viwango vya juu.

NA NEEMA MKUMBI - HUHESO DIGITAL KAHAMA



Naibu Waziri wa Nchi, TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amemtaka Mkandarasi anayetekeleza Mkataba wa Ujenzi wa miundombinu katika Mradi wa TACTIC wilayani Kahama kuhakikisha wanakamilisha ujenzi kwa haraka na kwa viwango vinavyotakiwa.


Mhe. Katimba amesema hayo leo Disemba 04, 2024 katika Manispaa ya Kahama Shinyanga, wakati wa utiaji saini mkataba wa Ujenzi wa Miradi wa Kituo Kikuu cha mabasi, Soko la Sango, na kituo kidogo cha Mabasi na Soko la Wajasiriamali wadogo katika eneo la Zongomela ni muhimu kwa uchumi wa wananchi na Mkoa wa Shinyanga.



Viongozi mkoani Shinyanga wamelalamikia kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi na mwendo wa Mkandarasi M/S Sichuan Road and Bridge Corporation Ltd, anayetekeleza ujenzi wa barabara na miundombinu mingine ya Mji wa Kahama.




Mhe. Katimba amekagua miradi hiyo na ameahidi kumshauri Waziri wa TAMISEMI kuhusu hatua stahiki dhidi ya Mkandarasi anayetekeleza miradi hiyo, akieleza kuwa kuchelewa kwa utekelezaji kunasababisha kupoteza tija ya uwekezaji.




Naibu Waziri ametoa maagizo kwa Mtaalamu Mshauri na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kahama kuhakikisha mikataba inasimamiwa vizuri ili kukamilisha miradi kwa ubora na katika muda uliopangwa ili kuondoa changamoto zinazotokana na ucheleweshaji wa utekelezaji.


Mhe. Katimba amezungumzia ongezeko la bajeti ya TARURA kutoka Bilioni 275 hadi Bilioni 710 kwa mwaka, akisisitiza kuwa uboreshaji wa miundombinu ya barabara ni muhimu kwa maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga.

Kwa upande wa wananchi wa Manispaa ya Kahama Gaudencia Tito amesema kituo hicho cha mabasi kitafungua fursa nyingi kwao kama biashara kwa wajasiriamali kwa kuwa kituo hicho kitakuwa kikubwa kuliko hiki cha sasa.



James Charles ameeleza kuwa kituo cha mabasi kilichopo sasa kina mlango mmoja tu ambao unatumika kuingiza mabasi na kutoka hivyo kituo hiki kilichosainiwa leo ni kikubwa na kinakidhi hadhi ya Manispaa.


Miradi hiyo inatarajiwa kusaidia kukuza uchumi wa Mkoa wa Shinyanga, kuboresha miundombinu na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi.



Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba, akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Kahama kuhusu changamoto za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara zinazojengwa na kampuni ya Cichwan Road and Bridge.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba, akikagua miradi ya ujenzi wa barabara
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba, akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Kahama kuhusu changamoto za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara zinazojengwa na kampuni ya Cichwan Road and Bridge.

Eneo la barabara inayojengwa katika Manispaa ya Kahama7


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zainab Katimba, akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Kahama kuhusu changamoto za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara zinazojengwa na kampuni ya Sichu0an Road and Bridge


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso