Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Makoye Peter Mayala (45), amejiua kwa kujinyonga baada ya kumjeruhi mtoto wake mwenye umri wa miaka 6 kwa kumkata shingoni kwa kutumia kitu chenye ncha kali.
Tukio hilo limetokea alfajiri ya leo, Desemba 2, 2024, baada ya mwanaume huyo kutokuwa na maelewano na mkewe (jina linahifadhiwa).
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, mkewe alikimbia nyumbani kutokana na mivutano ya kifamilia, na marehemu alichukua uamuzi wa kumjeruhi vibaya mtoto wake maeneo ya shingoni kabla ya kujinyonga.
Jeshi la Polisi mkoani humo limefika katika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa awali na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo na kuwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi wakati wanapokutana na changamoto za kifamilia.

No comments:
Post a Comment