John Mkama, Afisa Mahusiano wa KUWASA, akisisitiza umuhimu wa mkataba mpya katika kuboresha huduma ya maji na usafi wa mazingira, ili kukabiliana na changamoto zinazozuia upatikanaji wa huduma bora kwa wateja
NA NEEMA NKUMBI -HUHESO DIGITAL KAHAMA
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Kahama (KUWASA) leo, Desemba 2, 2024, imefanya kikao na wadau wake, kikiwa na lengo la kuwajulisha kuhusu mkataba wa huduma kwa wateja.
Mkutano huu umefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kahama kwa nia ya kuboresha huduma ya maji safi na usafi wa mazingira katika Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya Msalala.
Akizungumza katika kikao hicho, John Mkama, Afisa Mahusiano wa KUWASA, amesisitiza kuwa mkataba huu utaimarisha utoaji wa huduma bora ya maji na usafi wa mazingira kwani mkataba huo umelenga kuboresha huduma kwa wateja na kuondoa changamoto zinazozuia upatikanaji wa huduma bora.
Mkama ameeleza changamoto zinazokikabili kikosi cha KUWASA, ikiwa ni pamoja na wananchi kujiunganishia maji bila kibali na baadhi yao kutiririsha maji taka kwenye mitaro hasa wakati wa masika.
Changamoto nyingine ni wizi wa mita za maji, ambapo matukio 120 yameripotiwa ambapo hii inahitaji hatua za haraka za kuimarisha ulinzi na udhibiti wa huduma.
Diwani wa Kagongwa, Ismail Masolwa, ameshauri KUWASA kuweka mfumo wa malipo ya kabla katika ankara za maji kama ilivyo kwa huduma ya umeme kwa sababu mfumo huu utaondoa tatizo la wateja kutojali madeni ya ankara za maji, na hivyo kuboresha usimamizi wa fedha za mamlaka.
Aidha, Inspekta Hamis Nnunguye, Mkuu wa Upelelezi Msaidizi kutoka OCD, alifafanua kuwa wanaendelea na doria za ulinzi ili kudhibiti wizi wa mita za maji, na kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa zinakuwa salama kwa wananchi wote.
Kuwasa inahudumia wateja wapatao 34,021, kata 17 zilizopo Manispaa ya Kahama na 1 kutoka Halmashauri ya Msalala.
Wadau wa maji Manispaa ya Kahama wakiwa katika picha ya pamoja
Wadau wa maji Manispaa ya Kahama wakiwa katika picha ya pamoja
Wadau wa maji Manispaa ya Kahama wakiwa katika picha ya pamoja
John Mkama, Afisa Mahusiano wa KUWASA, akisisitiza umuhimu wa mkataba mpya katika kuboresha huduma ya maji na usafi wa mazingira, ili kukabiliana na changamoto zinazozuia upatikanaji wa huduma bora kwa wateja.
No comments:
Post a Comment