KAIMU MKUU WA MKOA SHINYANGA, MKUU WA MKOA TABORA AKABIDHI ZAWADI KWA WATOTO WA KITUO CHA MVUMA KAHAMA KWA AJILI YA SIKUKUU ZA MWAKA MPYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 28 December 2024

KAIMU MKUU WA MKOA SHINYANGA, MKUU WA MKOA TABORA AKABIDHI ZAWADI KWA WATOTO WA KITUO CHA MVUMA KAHAMA KWA AJILI YA SIKUKUU ZA MWAKA MPYA

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, amekabidhi zawadi kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Mvuma kilichopo Manispaa ya Kahama kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya.

NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL KAHAMA

Katika hatua za kuadhimisha sikukuu za Krismas na mwaka mpya, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, amekabidhi zawadi kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Mvuma kilichopo Manispaa ya Kahama kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya.

Zawadi hizo, ambazo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan, zimetolewa mnamo Disemba 27, 2024, Lengo kuu ni kuhakikisha watoto hao wanasherehekea sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya kwa furaha na kujisikia kuwa sehemu ya jamii.

Kaimu Mkuu wa Mkoa, Paul Chacha, amesema kuwa Rais Samia alitoa maelekezo kwa kila wilaya kutoa msaada kwa watoto wanaolelewa katika vituo mbalimbali ili kuondoa hisia za upweke na kuongeza furaha kwa watoto wanaohitaji msaada katika kipindi hiki cha sikukuu.

Pia, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Masudi Kibetu, amesema kwamba Kituo cha Mvuma kinamilikiwa na Manispaa ya Kahama kwa sasa kina watoto 40, ambapo wasichana ni 26 na wavulana 14, Kati ya watoto hao, 25 wanahudhuria shule.

Masudi ametoa wito kwa jamii kuungana na Rais Samia katika kuwakimu watoto wenye uhitaji ili nao wafurahi kama wenzao, huku akisisitiza umuhimu wa jamii kuacha vitendo vya kikatili dhidi ya watoto.

Mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Mvuma, Victoria Justin, alieleza furaha yake kutokana na zawadi hizo, na kumshukuru Rais Samia kwa msaada na ushirikiano wa serikali katika kuhakikisha watoto wana furaha kama wenzao.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyakato, Kata ya Nyasubi, Husein Mwita, amewahimiza wadau na watu binafsi kutoa misaada kwa watoto wasiojiweza huku akimshukuru Rais Samia kwa msaada huo ambao umeleta faraja kwa watoto wa kituo hicho.

Naye Kiongozi wa Kituo cha Mvuma, Laurine Noel, ametoa shukrani kwa Rais Samia kwa msaada huo, na akaomba serikali kuajiri wafanyakazi wa kudumu katika kituo hicho kwani kwa sasa, wafanyakazi wanajitolea.

Laurine ameeleza changamoto wanazokutana nazo, ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa wataalamu wa kushughulikia watoto wenye matatizo ya akili, na kuomba serikali kuwaletea wataalamu wa afya ya akili ili kusaidia watoto hao.
watoto wa kituo cha mvuma wakipiga picha ya pamoja na viongozi waliotembelea kituo hicho kwa ajili ya kukabidhi zawadi ambazo nimaelekezo ya Rais Samia 

watoto wa kituo cha mvuma wakipiga picha ya pamoja na viongozi waliotembelea kituo hicho kwa ajili ya kukabidhi zawadi ambazo nimaelekezo ya Rais Samia

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, amekabidhi zawadi kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Mvuma kilichopo Manispaa ya Kahama kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, amekabidhi zawadi kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Mvuma kilichopo Manispaa ya Kahama kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso