INEC YASISITIZA UWAZI UBORESHAJI WA DAFTARI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 16 December 2024

INEC YASISITIZA UWAZI UBORESHAJI WA DAFTARI





Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati wa mafunzo kwa watendaji wa ubioreshaji ngazi ya Mkoa kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoa wa Mbeya uliofanyika leo Desemba 16, 2024.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele (kushoto) akizungumza jambo wakati wa mafunzo kwa watendaji wa ubioreshaji ngazi ya Mkoa kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoa wa Mbeya uliofanyika leo Desemba 16, 2024. Pamoja nae ni Mkurughenzi wa Uchaguzi wa INEC, Bw. Kailima Ramadhani.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele (katikati) akizungumza jambo wakati wa mafunzo kwa watendaji wa ubioreshaji ngazi ya Mkoa kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoa wa Mbeya uliofanyika leo Desemba 16, 2024. Kulia ni Mjumbe wa INEC, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar na kushoto ni Mkurughenzi wa Uchaguzi wa INEC, Bw. Kailima Ramadhani.

Mrakibu msaidizi wa Uhamiaji Gerhard Mardai akiwasilisha mada kuhusua uaraia wakati wa mafunzo hayo.

Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.

Na Mwandishi Wetu
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imesema uwepo wa mawakala kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura ni kielelezo cha uwazi kwenye zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.


Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari ngazi ya mkoa mkoani Mbeya, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amesema pamoja na kuhakikisha zoezi linafanyika kwa uwazi mawakala hapo pia watasaidia kuwatambua wananchi wanaoomba kuandikishwa.


“Wakati wa uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura. Jambo hili ni muhimu kwani litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima,” amesema Jaji Mwambegele.


Ameongeza kuwa mawakala hao hawaruhusiwi kuwaingilia watendaji wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao vituoni.


Akizungumza wakati wa kufungua mkutano kama huo mkoani Iringa, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk amesema katika kuhakikisha zoezi hilo linakuwa la uwazi Tume imetoa kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari kwa asasi za kiraia 157 na asasi za kiraia 33 kwa ajili ya uangalizi wa zoezi hilo.


“Ni muhimu kutoa ushirikiano kwa asasi hizo zitakapofika kwenye maeneo yenu kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao. Tume itawapa vitambulisho kwa urahisi wa kuwatambua,” amesema Jaji Mbarouk.


Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari mkoani Mbeya, Iringa na mkoa wa Dodoma kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ambapo uboreshaji utafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 27 Desemba, 2024 hadi tarehe 02 Januari, 2025 na vituo vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk amefungua mafunzo kwa watendaji wa uboreshaji ngazi ya mkoa, Mkoani Iringa leo Desemba 16, 2024 ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Uboreshaji huo utafanyika Mkoani Mbeya, Iringa na mkoani Dodoma kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuanzia tarehe 27 Desemba, 2024 hadi tarehe 02 Januari, 2025 ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za sheria, Selemani Mtibora akizungumza jambo wakati wa mafunzo mkoani Iringa.


Washiriki wa Mkoa wa Iringa wakifuatilia mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa uboreshaji ngazi ya Mkoa kutoka halmashauri zote za mkoa wa Iringa wakila kiapo cha kujitia uanachama na kutunza siri kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo leo Desemba 16, 2024.

Washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa uboreshaji ngazi ya Mkoa kutoka halmashauri zote za mkoa wa Mbeya wakila kiapo cha kujitia uanachama na kutunza siri kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo leo Desemba 16, 2024. Walikula kiapo mbele ya Hakimu Mkazi wea Mahakama ya Mwanzo Mbeya, Mhe, Upendo Moshi.


Washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa uboreshaji ngazi ya Mkoa kutoka halmashauri zote za mkoa wa Mbeya wakila kiapo cha kujitia uanachama na kutunza siri kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo leo Desemba 16, 2024. Walikula kiapo mbele ya Hakimu Mkazi wea Mahakama ya Mwanzo Mbeya, Mhe, Upendo Moshi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso