AFARIKI DUNIA AKIOGELEAKATIKA BWAWA LA KUOGELEA SIKU YA KRISMAS KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 27 December 2024

AFARIKI DUNIA AKIOGELEAKATIKA BWAWA LA KUOGELEA SIKU YA KRISMAS KAHAMA

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza na waandishi wa habari disemba 27, 2024 ofisini kwake, akielezea tukio la kijana kupoteza maisha  akiogelea katika bwawa la kuogelea

NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL KAHAMA


Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mbaraka Magese (24) amefariki dunia wakati akiogelea katika bwawa la kuogelea la Bar ya Nzengo Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga.


Tukio hilo limetokea Disemba 25, 2024 majira ya saa moja usiku, Mbaraka alikuwa akiogelea katika bwawa hilo huku mvua ikinyesha hali iliyopelekea kushindwa kuogelea na kuanza kuzama ambapo alitolewa na kupelekwa hospitali na kupoteza maisha wakati akipatiwa matibabu.


Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita amesema kuwa wamiliki wa mabwawa ya kuogelea wanapaswa kuzingatia sheria na kanuni zinazohusiana na uendeshaji wa mabwawa ili kuepuka majanga kama hayo.


Kamati ya Usalama Wilaya ya Kahama, chini ya uongozi wa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, imelaani tukio hilo na kutoa tamko rasmi kwamba bar hiyo imefungwa kutokana na kutokidhi vigezo vya usalama katika huduma za kuogelea.


Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, Stanley Luhwago, amesema wasimamizi wa mabwawa hayo lazima wawe na ujuzi wa kuogelea pia kuwe na vifaa vya kuogelea kama jaketi na maboya ili kuhakikisha usalama kwa waogeleaji kwani wako wengine hawajui kuogelea kabisa.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga RPC Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba chanzo cha kifo cha kijana huyo ni kumeza maji mengi wakati akiogelea huku mvua ikinyesha hivyo wanamshikilia msimamizi wa bwawa kwa uchunguzi zaidi.


Kamanda amewataka wamiliki kuwa waangalifu pia kufunga mabwawa ya kuogelea wakati mvua ikinyesha ili kuepusha madhara kama haya.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso