Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, akitoa wito kwa Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa serikali za mtaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
NA NEEMA NKUMBI- HUHESO DIGITAL USHETU
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa serikali za mtaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Mboni ametoa wito huo Novemba 7, 2024, wakati wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Ushetu ambapo amesisitiza kuwa wananchi walihamasishwa kwa siku 10 kujiandikisha, na sasa wanahitajika kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi, Novemba 27, 2024.
DC Mboni amesema kwamba Uchaguzi huu ni muhimu kwa maendeleo ya kijamii, hivyo ni jukumu la madiwani kuhakikisha kwamba wananchi wanahamasika na wanajua umuhimu wa kuchagua viongozi bora wa serikali za mtaa.
Diwani wa Kata ya Nyamilangano Robart Maganga amesisitiza umuhimu wa uchaguzi huu kwa maendeleo ya wananchi na akawahimiza madiwani kuongeza juhudi katika kuhakikisha wananchi wanajitokeza kupiga kura.
Mkuu wa Wilaya, Mboni Mhita, pia aliwahimiza madiwani kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ujio wa madaktari bingwa wa Mama Samia, ambao wamekuja kwa lengo la kusogeza huduma za afya kwa wananchi katika maeneo yao.
Mboni ameeleza kuwa Rais Samia ameamua kusogeza huduma za madaktari bingwa kwa maeneo mbalimbali, ambapo madiwani wanahitajika kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi kuhusu ujio wa madaktari hao, ambao wataweza kutoa uchunguzi wa awali wa magonjwa na kusaidia katika matibabu mapema.
Diwani wa Kata ya Nyamilangano, Robart Maganga, akisisitiza umuhimu wa uchaguzi huu katika kukuza maendeleo ya wananchi na kuhimiza madiwani kuongeza juhudi za kuhakikisha wananchi wanajitokeza kupiga kura.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, akitoa wito kwa Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa serikali za mtaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
No comments:
Post a Comment