Kamishna wa Viapo, Stephen Magalla, akiwaapisha wenyeviti wa serikali za mitaa leo novemba 29, 2024, Kahama.
NA NEEMA NKUMBI- HUHESO DIGITAL KAHAMA
Wenyeviti wapya wa serikali za mitaa katika Manispaa ya Kahama wameapishwa rasmi leo, Novemba 29, 2024, na Kamishna wa Viapo, Stephen Magalla, katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya John Paul Wapili, Kahama.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Masudi Kibetu, amewapongeza wenyeviti wapya kwa kuchaguliwa na wananchi kwa kusema kuwa uteuzi wao ni ishara ya imani kubwa waliyopewa na jamii, hivyo inapaswa kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa na bila upendeleo.
Masudi amesisitiza umuhimu wa viongozi hao kuzingatia sheria na kanuni katika utendaji wao wa kazi, pia amewataka viongozi hao kuwa waadilifu, kuepuka rushwa, na kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi.
Wenyeviti wa serikali za mitaa wameeleza dhamira yao ya kufanya kazi kwa uwazi na ufanisi huku wakisisitiza kwamba watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa manufaa ya wananchi, wakizingatia maslahi ya watu wao na kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa usawa.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwime kata ya Mwendakulima, Stella Maige akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya Kuapishwa

Akizungumza kwa niaba ya wenyekiti mara baada ya kuapishwa Fadhili Wakuyamba, ameahidi kufanya vizuri zaidi kuliko wakati uliopita huku akijiepusha na rushwa.
Wenyeviti wa Serikali za mitaa na wajumbe wakiapa mbele ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Masudi Kibetu

Masudi akisisitiza umuhimu wa viongozi kuzingatia sheria, kuwa waadilifu, na kuepuka rushwa katika utendaji wao wa kazi, ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wananchi.

No comments:
Post a Comment