WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MADINI NA UWEKEZAJI 2024. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 19 November 2024

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MADINI NA UWEKEZAJI 2024.



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 19, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji Tanzania, kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.


Mkutano huo unawakutanisha wadau wa madini wanaojishughulisha na utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani madini, wasimamizi wa Sekta kutoka Serikalini, watoa huduma migodini na wafanyabiashara.


Pamoja na malengo mengine, mkutano huo umelenga kuweka mipango ya kuvutia uwekezaji wa nje ya nchi, kukuza usimamizi bora wa rasilimali za Madini pamoja na kubadilishana uzoefu na washiriki kutoka maeneo mbalimbali duniani.


Kaulimbiu ya mkutano huo ni _Uongezaji wa Thamani ya Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi_






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso