Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe .Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasili Harare, Zimbabwe, tarehe 16 Novemba, 2024 kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 17 - 19 November 2024.
Waziri Kombo amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. IGP Mstaafu Simon Sirro.
Pia, Mhe. Kombo amekutana na Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki mkutano huo na kupokea taarifa ya maandalizi ya mkutano huo ambao unalenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu kanda hiyo hususan hali ya Ulinzi, Usalama na mikakati ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba kanda.
Aidha mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa Kamati ya Makatibu wakuu wa SADC utakaofanyika tarehe 17 November 2024.
No comments:
Post a Comment