Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Hamad Mbega, akisisitiza haki ya kukata rufaa kwa wagombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Muda wa kupokea rufaa ni kuanzia Novemba 10 hadi Novemba 13, 2024.
NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL KAHAMA
Wagombea kutoka chama cha upinzani Chadema wamedai kuenguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Kitongoji na Vijiji wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, licha ya kufuata taratibu zote za kisheria na kanuni za uchaguzi. Madai hayo yamewasilishwa leo, Novemba 12, 2024, wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
Wakizungumza katika mkutano huo, viongozi wa Chadema wamesema kuwa majina ya wagombea yanaondolewa na watendaji wa serikali za mitaa kwa sababu zisizo na msingi, jambo ambalo linakiuka kanuni za uchaguzi zinazozuia kuingiliwa kwa mchakato wa uchaguzi.
Mwenyekiti wa kamati ya Chadema ni msingi Kanda ya Serengeti, Juma Protas, amesema kwamba Tanzania ni nchi ya amani na siasa zinapaswa kufanywa kwa utulivu pia ametaka mamlaka zinazohusika na usimamizi wa uchaguzi kutekeleza sheria na kanuni ili wagombea waliostahili waweze kugombea na walio na sifa wachaguliwe na wananchi.
Kwa upande mwingine, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Hamad Mbega, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, amewahakikishia wagombea kwamba watakuwa na haki ya kukata rufaa kwa maamuzi ya watendaji wa uchaguzi.
Mhe, Mbega ameongeza kuwa muda wa kupokea rufaa ni kuanzia Novemba 10 hadi Novemba 13, 2024, na amewataka wale wanaopinga maamuzi ya uchaguzi kuwasilisha rufaa zao kwa wakati ili kufanya mchakato wa kupitia vielelezo na kutoa maamuzi ya haki.
'Wasilisheni rufaa zenu kwa wakati ili kuhakikisha mchakato unafanyika kwa haki,' asema Mbega."
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Hamad Mbega, akisisitiza haki ya kukata rufaa kwa wagombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Muda wa kupokea rufaa ni kuanzia Novemba 10 hadi Novemba 13, 2024.
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti, Juma Protas, akizungumza kuhusu umuhimu wa amani na utulivu katika siasa, akisisitiza kuwa mamlaka zinazohusika na uchaguzi ziweze kutekeleza sheria na kanuni ili wagombea waliostahili wachaguliwe na wananchi wachaguliwe
Viongozi wa Chadema wakidai kuwa majina ya wagombea yanaondolewa bila msingi, jambo linalokiuka kanuni za uchaguzi zinazozuia uingiliaji.
No comments:
Post a Comment