TANZANIA NA CHINA ZAZUNGUMZIA UTEKELEZAJI WA USHIRIKIANO WA MAENEO 10 YA MKUTANO WA FOCAC. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 13 November 2024

TANZANIA NA CHINA ZAZUNGUMZIA UTEKELEZAJI WA USHIRIKIANO WA MAENEO 10 YA MKUTANO WA FOCAC.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo katika mazungumzo ya utekelezaji wa maeneo 10 ya ushirikiano kati ya China na Afrika, Tanzania ikiwemo kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China katika Mkutano wa FOCAC uliofanyika mwezi Septemba 2024 jijini Beijing, China.


Hayo yamebainishwa katika kikao kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel W. Shelukindo na Bw. Du Xiaohui, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China na Katibu Mkuu wa Kamati ya Ufuatiliaji ya China ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kilichofanyika tarehe 11 Novemba 2024 jijini Dar es Salaam.


Halikadhalika, wawili hao walijadili kuhusu ufufuaji wa reli TAZARA na umuhimu wake katika kukuza uchumi wa Tanzania na Zambia kwa kukuza uwekezaji na biashara ikiwa ni pamoja na kuongeza biashara kati ya Tanzania na China.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso