Mwenyekiti wa asasi ya siasa, ulinzi na usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amezisisitiza nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kuunga mkono juhudi za kidiplomasia za kumaliza Uhasama uliopo baina ya DRC na Rwanda chini ya mchakato wa Angola.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo kwa niaba ya Rais Dkt.Samia alipomwakilisha kufungua Mkutano wa Viongozi Wakuu na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika uliofanyika jijini Harare Zimbabwe tarehe 20 Novemba 2024.
Rais Dk, Samia amefafanua kuwa wakati nchi za SADC zikiendelea kujadili hali ya Usalama wa Mashariki ya DRC ni vyema kukawekwa mifumo imara ya Ufuatiliaji na utekelezaji wa maazimio yanayoidhinishwa na Jumuiya mbalimbali za Kikanda ikiwemo yale ya Umoja wa Afrika(AU) na Umoja wa Mataifa (UN).
Ameeleza kuwa hatua hiyo itawezesha kupatikana kwa Misaada ya kifedha na kilojistik kwa wakati na kuongeza Ufanisi wa Misheni za SADC na kupunguza gharama.
Rais Dk, Samia amezishauri nchi za SADC kutumia majadiliano ya Mkutano huo kutoka na maazimio yatakayokuwa chachu ya kupatikana kwa Amani ya kudumu katika Ukanda wa SADC na kuwa ni ushahidi wa dhamira ya nchi hizo ya kuleta Amani Endelevu.
No comments:
Post a Comment