Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama, Thomas Muyonga, awataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kutatua changamoto za wananchi na kusimamia rasilimali kwa ufanisi.
NA NEEMA NKUMBI-HUHESO DIGITAL KAHAMA
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama, Thomas Muyonga, amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kusimamia rasilimali za mitaa ili kutekeleza ilani ya chama.
Nasaha hizo amezitoa Novemba 29, 2024, kwenye viwanja vya CCM, ambapo amesisitiza umuhimu wa kushirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo na kuhimiza utawala bora.
Muyonga amesema, "Tunakwenda kufanya kazi, katatueni kero za wananchi, simamieni rasilimali za mitaa yenu na kushirikiana na wananchi ili wanufaike na utawala wao."
Muyonga ameongeza kuwa viongozi wanapaswa kudumisha umoja, mshikamano, na kuunganisha wananchi ili kuepuka kuwa kikwazo cha maendeleo.
Kwa upande mwingine, Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Mfaume Kizigo, amesisitiza umuhimu wa kusimamia 4R za Mama Samia, akisema kwamba kudumisha maridhiano na uelewano kutasaidia nchi kuendelea kuwa na amani.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Mfaume Kizigo, asisitiza umuhimu wa kusimamia 4R za Mama Samia, akisema kuwa maridhiano na uelewano ni muhimu kwa kudumisha amani na maendeleo ya nchi
Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Joachim Simbila akizungumza na wenyeviti wa serikali za mitaa

No comments:
Post a Comment