MAJALIWA ATAKA SEKTA YA MADINI KUWA NA TIJA KIUCHUMI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 19 November 2024

MAJALIWA ATAKA SEKTA YA MADINI KUWA NA TIJA KIUCHUMI



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kuiunga mkono sekta ya madini lengo likiwa ni kuona sekta hiyo inakuwa kwa kasi na tija kwa uchumi wa nchi.
Majaliwa ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Sita wa Kimataifa wa Madini ulioanza leo na unatarajiwa kumalizika Alhamisi.

Majaliwa amesema serikali imeimarisha sekta hiyo kwa kuongeza uwezo wa nishati ya umeme, kuimarisha njia ya usafirishaji kwa kuboresha barabara ya usafirishaji wa madini hayo , kuongeza ndege ili kuimarisha sekta hiyo kwani ni nguzo muhimu kwa ukuaji wa uchumi kwenye nchi yetu.

Majaliwa amesema mkutano huo utaonesha teknolojia rafiki kwa mazingira kwenye uchimbaji madini malengo kuvutia uwekezaji kutoka nje kuja nchini ili iweze kuongeza sekta ya madini kukua hapa nchini, kubadlishana mawazo , kukuza usimamizi bora wa rasilimali tulizonazo za madini kwa manufaa ya taifa letu , kuongeza fursa za ajira na kuboresha ustawi wa jamii unaozunguka kwenye uchimbaji wa madini , kuimarisha ushirikiano kati ya serikali mbalimbali sekta binafsi na wadau wengine.


Imeandaliwa na Samuel Swai

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso