MADAKTARI BINGWA KUONGEZA MOLARI KWA WANANCHI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 13 November 2024

MADAKTARI BINGWA KUONGEZA MOLARI KWA WANANCHI



Na WAF - Geita, Katoro


Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Geita, Dkt. Modest Buchard amesema miongoni mwa faida ya kambi ya matibabu ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia nikuongeza molari na hamasa kwa wananchi kuipenda Serikali yao.


Dkt. Buchard ameyasema hayo Novemba 12, 2024 mkoani Geita katika hospitali ya Katoro kwenye kambi ya matibabu ya madaktari bingwa wa Rais Samia itakayokuwepo kwa siku sita (6) mkoani humo.


"Kupelekwa kwa madaktari bingwa katika halmashauri inachochea wananchi kuona kuwa Serikali ya nchi yao inawajali kwa kuwapatia huduma za kibingwa katika maeneo yao na kwa gharama nafuu," amesema Dkt. Buchard na kuongeza


“Madaktari bingwa hawa wanafanya kazi nzuri sana kwani mpaka sasa wameona zaidi ya wananchi 50, hizi kambi zina faida nyingi kwa wananchi hususan wale wanaoshindwa kusafiri kwenda kufuata huduma za kibingwa katika hospitali za mikoa, taifa na kanda hivyo wanazipata karibu na maeneo yao,” amesisitiza Dkt. Buchard.


Dkt. Buchard ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kutoa kiasi cha Shilingi za kitanzania Bilioni 500 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa miradi ya jengo la watoto, wakina mama, wanaume na nyumba ya maiti.


“Tunashukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia kwa kutujengea hospitali hii ya Katoro iliyogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 3.5 ambayo imekamilika na wameshatupatia Shilingi Bilioni 500 ambazo zitatumika kumalizia jengo la watoto, mama, wanaume na maiti,” amesema Dkt. Buchard.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso