CCM MSALALA YAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KATIKA KATA YA ISAKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 20 November 2024

CCM MSALALA YAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KATIKA KATA YA ISAKA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama, Thomas Muyonga, amezindua rasmi kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kata ya Isaka, Halmashauri ya Msalala, huku akihudhuriwa na mamia ya wafuasi na viongozi wa chama, Novemba 20, 2024.

NA NEEMA NKUMBI -HUHESO DIGITAL MSALALA


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Kahama, Thomas Muyonga leo novemba 20, 2024 amezindua rasmi kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Kata ya Isaka Halmashauri ya Msalala na kuhudhuriwa na mamia ya wafuasi na viongozi wa chama.


Akizungumza mbele ya umati wa wananchi, Mheshimiwa Thomas amesisitiza amani na utulivu wakati wote wa kampeni mpaka siku ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika novemba 27, 2024.

"Kipindi hiki cha uchaguzi lazima tuhakikishe amani inatawala, swala la amani sio mchezo tusiruhusu mtu yeyote kuharibu amani yetu hivyo katika kampeni hizi tutahubiri maendeleo tuliyoyafanya na tutakayoyafanya", amesema Thomas.

Aidha Mbunge wa jimbo la Msalala Mheshimiwa Idd Kasimu Idd amesema Wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji ndio wenye majukumu ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali katika ngazi ya kijiji hivyo hawa ndio injini katika serikali za mitaa.

"Ili mimi niweze kutekeleza majukumu na kuona fedha ambazo Dkt. Samia anatupatia zinahitaji usimamizi wa hawa wenyeviti wa mitaa na vijiji, halafu pia hawa ndio majukumu ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo maana yake tunapohitaji zahanati katika kijiji mwenyekiti ndie anaeibua",amesema mheshimiwa Idd.

"Viongozi mtakaochaguliwa nendeni mkafanya kazi kama timu kwani CCM ni timu moja", ameongeza mheshimiwa Idd

Kampeni hizi zimezinduliwa rasmi leo, Novemba 20, 2024, zinatarajiwa kuendelea hadi Novemba 26, 2024, kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa kufanyika Novemba 27, 2024.

Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mheshimiwa Idd Kasimu Idd, akisisitiza umuhimu wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji katika kuibua na kubuni miradi mbalimbali, akisema wao ndio injini kuu katika maendeleo ya serikali za mitaa.
Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mheshimiwa Idd Kasimu Idd, akisisitiza umuhimu wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji katika kuibua na kubuni miradi mbalimbali, akisema wao ndio injini kuu katika maendeleo ya serikali za mitaa.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama, Thomas Muyonga, akizindua rasmi kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kata ya Isaka, Halmashauri ya Msalala, huku akihudhuriwa na mamia ya wafuasi na viongozi wa chama, Novemba 20, 2024
Katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kahama akitoa salamu wakati wa uzinduzi wa kampeni  

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso