Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Deogratius Ndejembi akiipongeza juhudi za usimamizi mzuri wa ujenzi wa vyumba vya madara katika shule ya sekondari Mapamba
NA NEEMA NKUMBI- HUHESO DIGITAL MSALALA
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Deogratius Ndejembi ameanza ziara yake ya kikazi wilayani Kahama leo octoba 6, 2024 ambapo atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo.
Ziara hiyo ya siku mbili imeanzia halmashauri ya Msalala ambapo ametembelea shule ya sekondari Ntobo kukagua vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo ambapo amesema hajabaini kasoro yoyote katika ujenzi huo.
Mheshimiwa Ndejembi ameipongeza Halmashauri ya Msalala kwa usimamizi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Ntobo kwani madara hayo yana ubora unaoendana na thamani ya fedha pia kubakiwa na zaidi ya shiling milion 10.
"tumetembelea na kukagua madarasa haya sijaona kasoro yoyote katika utekelezaji wa mradi huu, shule ina ubora unaoendana na thamani ya pesa na mmebakiwa na zaidi ya Mil. 10 nawapongeza kwa usimamizi mzuri wa fedha," amesema Mhe. Ndejembi.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa madarasa, Mkuu wa Shule ya Sekondari Ntobo Sekondari Mwalimu Hussein Mbwambo amesema ujenzi wa madarasa 7 umegharimu shilingi 170,892, 221.49 pia matundu 8 ya vyoo vyenye gharama ya sh13459550 na ofisi 1 na kubakiwa na zaidi ya Sh. Milioni 12 ambapo wamemuomba Mkurugenzi wa Halamshauri ya Msalala kuwaruhusu zitumike kukarabati jengo la utawala.
Aidha Mkuu wa mkoa Shinyanga Anamringi Macha amemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo katika Mkoa wa shinyanga pia kwa sasa hakuna utofauti wa miundo binu kati ya mjini na vijiini, Shule za vijijin nazo zimeboreshwa miundombinu yote muhimu ya watu
Ujenzi wa Ntobo .
Naye Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Iddy Kassim amewataka uongozi wa shule hiyo kutunza miundo ya madarasa viti pamoja na vyoo kwani vimetumia gharama kubwa
Shule ya Sekondari Ntobo ilianzishwa mwaka 2006, ni shule ya kutwa ambayo ni mchanganyiko wa wavulana na wasichana ambayo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 577 na bweni la wanafunzi wa kike lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 48.
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Deogratius Ndejembi akiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Deogratius Ndejembi akiipongeza Halmashauri ya msalala kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa vyumba vya madara katika shule ya sekondari Ntobo
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Deogratius Ndejembi akiipongeza Halmashauri ya msalala kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa vyumba vya madara katika shule ya sekondari Ntobo
Huu ndio muonekano wa vyumba vya madarasa saba vilivyojengwa katika shule ya sekondari Ntobo
Madawati yaliyopo kayika vyumba vipya vya madarasa
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ntobo Mwalimu Hussein Mbwambo akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo.
No comments:
Post a Comment