Mkurugenzi wa taasisi ya simama tena akizungumza katika kikao kilicholenga kutambulisha taasisi hiyo pamoja na nyumba ya upataji nafuu sober house na kutoa tathmini juu ya utafiti na uelewa wa madawa ya kulevya katika makundi sita waliyoyafanyia urafiti.
NA NEEMA NKUMBI -HUHESO DIGITAL KAHAMA
Wazazi na walezi waaswa kitenga muda kwa ajili ya vijana na kuwapa malezi yawapasayo ilikuepuka kuendelea kuongezeka kwa Waraibu wa madawa ya kulevya nchini.
Hayo yamesemwa octoba 17, 2024 na Mkurugenzi wa Taasisi ya SIMAMA TENA (STF) Grace Paul Nzagamba katika kikao kilichokuwa na lengo la uzinduzi wa taasisi hiyo pamoja uzinduzi wa Nyumba ya upataji nafuu kwa waraibu wa dawa za kulevya (SOBER HOUSE).
Grace amesema walifanya tafiti kwa makundi sita juu ya uelewa wa dawa za kulevya yakiwemo, walimu, wanafunzi, wazazi, warahibu wenyewe,waandishi wa habari pamoja na viongozi wa dini, wamebaini kuwa vijana wengi wanaathirika na dawa hizo ikiwemo wanafunzi.
Naye msaikolojia katika SOBER hiyo Maria Affleck amesema wanawapokea warahibu wa dawa za kulevya na kuwatibu pia kuwapa ushauri nasaha ili kuachana na dawa za kulevya na kurudi katika hali yao ya kawaida.
Mmoja wa waraibu wa dawa za kulevya Ally Baden ambaye kwa sasa ni meneja wa Simama tena na Sober house amesema Mungu anampenda sana kwani wakati anatumia dawa za kulevya alikuwa anajihusisha pia na wizi ambao ulipelekea rafiki zake hata ndugu yake wa damu kufa hivyo aliamua kuacha kutumia madawa na kwenda kukaa katika sober house na sasa ni mtu mzuri.
Taasisi ya Simama Tena na Sober house iko Manispaa ya Kahama na imesajiliwa kisheria, pia kwa sasa Sober house hiyo inauwezo wa kuhudumia waraibu wapatao 20.
No comments:
Post a Comment