Waumini wa dini ya kiislamu wamekumbushwa kufanya mahafali ya kidini kwa vijana wao pia kuwafanyia dua kwa ajili ya mtihani kwani katika chumba cha mtihani kuna mengi.
Hayo yamesemwa octoba 20, 2024 na Sheikh Ramadhan Damka katika mahafali ya kidini ya kiislamu ambapo amesema viongozi wa dini yaa kiislamu washirikiane na waumini kujenga maadili ya watoto wao wakiwa shuleni.
Akizungumza katika mahafali hayo mwalimu Daud Mashafa Msekwa mwakilishi wa mgeni rasmi Mwalimu John Paul, amewakumbusha wanafunzi hao kasali kwani kusali sio ushamba.
"Nawakumbusha kusali kwani kusali sio ushamba ukisubili kusali kukizeekaa unaweza kuondoka ungali kijana", amesema Mwalimu Daud.
Mwalimu Daud ameongeza kwamba wazazi wanamchango mkubwa katika maadili ya watoto kwani kipindi hiki cha utandawazi ni kipindi kigumu sana katika malezi.
Akisoma risala iliyoandaliwa na wanafunzi Hadija Jabiri amesema katika kipindi cha miaka minne shuleni wamefanikiwa kusoma maarifa ya uislamu na baadhi ya shule kufanya mitihani ya elimu ya dini.
Katika risala hiyo wamebainisha changamoto mbalimbali ambazo ni ukosefu wa fedha za kuwalipa walimu wanaojitolea kuwafundisha, upungufu wa vitabu vya dini na ukosefu wa gharama za uzalishaji wa vitini vya nukuu za somo la dini EDK.
Akijibu risala Sheik Abdilah Yusuf (Sheikh Daruweshi) amesema waumini wapaswa kuanzisha mfuko kwa ajili ya kuwawezesha walimu wanaotoa elimu ya dini kwa vijana wao.
No comments:
Post a Comment