SHULE YA GREEN STAR SECONDARY YAFANYA MAHAFALI YA KWANZA TANGU KUANZISHWA KWAKE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 13 October 2024

SHULE YA GREEN STAR SECONDARY YAFANYA MAHAFALI YA KWANZA TANGU KUANZISHWA KWAKE


NA NEEMA NKUMBI-HUHESO DIGITAL


Wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne mwaka huu 2024 wameaswa kuwa na matumizi mazuri ya simu zao kwa wimbi kubwa la vijana limeharibiwa na utandawazi kwa kuiga mambo mbalimbali yasiyofaa.


Hayo yamesemwa na mgeni rasmi Charles Machali Oktoba 12, 2024 katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Green Star iliyopo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga ambapo amesema wanafunzi hao wakawe mabalozi wazuri kwa wazazi wao yale waliyojifunza shuleni.


Amesema wazazi wao wametumia gharama kubwa kuwasomesha hivyo itakuwa haina maana kuona vijana wao wakiharibika kwa kuiga mambo yasiyofaa kwa ikiwemo kujiingiza kwenye makundi ya madawa ya kulevya sambamba na starehe.


Machali amesema dunia ya sasa imekuwa ya kisasa (teknorojia) hivyo kuna mambo mengi ambayo yanafanyika katika mitandao ya kijamii kwahiyo wanapaswa kutokuiga mabaya kwani wazazi wao wanatarajia kulipwa na shukrani za watoto kwa kufanikiwa na sio kuharibika kwa makundi yasiyokuwa na maana.


"Niwaombe vijana mkafanye mambo ambayo wazazi wanatarajia kuyaona kwenu kwani wametumia gharama kubwa kuwasomesha sasa mkienda kujiingiza kwenye makundi ya hovyo kama vile disco, kuvuta bangi mtawakosea wazazi wenu".


"Watoto wa kike mkawe waadilifu sana msikimbilie chips, kama una hamu na chips mwambie mzazi wako naomba chips atakununulia kwani kama ameweza kukusomesha kwa gharama kubwa hashindwi kukununulia chips ya 2,000". alisema machali.


Kwa upande wake meneja wa shule hiyo ya Green Star, Petro Naftali amewataka wanafunzi wanaohitimu kuendeleza nidhamu waliyotoka nayo shuleni hapo kwani maisha yanaendelea huku akiwashukuru wazazi kwa ushirikiano wao ambao umewezesha kuwa na maendeleo mazuri kwa watoto shuleni hadi nyumbani.


Aidha wanafunzi wanaohotimu kidato cha nne katika shule hiyo kwa mwaka 2024 ni 44 ikiwa ni mahafali ya kwanza kwa shule hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 2021 na mwaka huu imekuwa na matokeo mazuri kwenye mtihani wa kujipima ikishika nafasi ya pili kiwilaya.





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso