WAHITIMU WA CHUO CHA THERAPON SHINYANGA WASISITIZWA KUENEZA NENO LA MUNGU KATIKA MAHAFALI YA PILI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 26 October 2024

WAHITIMU WA CHUO CHA THERAPON SHINYANGA WASISITIZWA KUENEZA NENO LA MUNGU KATIKA MAHAFALI YA PILI

Baadhi ya wanafunzi waliohitimu masomo ya dini ya Kikristo ya Theolojia katika ngazi tofauti wakiingia katika ukumbi


NA NEEMA NKUMBI -HUHESO DIGITAL SHINYANGA


Mahafali ya pili ya Chuo Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Shinyanga) yamefanyika leo, Oktoba 26, 2024, huku wahitimu 10 wakipata Shahada za Awali, ya Uzamili, na Shahada ya Umahiri katika masomo ya Theolojia.


Mgeni rasmi, Askofu Mstaafu Dkt. Emmanuel Makala, amewataka wahitimu kutumia elimu yao kueneza Neno la Mungu, akirejelea Mathayo 28:19-20 amekemea mmomonyoko wa maadili na kusisitiza umuhimu wa kuzuia ndoa za jinsia moja.


Dkt. Kulwa Meshack, Mratibu wa Mafunzo, amewasisitizia wahitimu kuwa chumvi na nuru ya ulimwengu, huku akihimiza umuhimu wa kuhubiri Injili na kutoa mchango chanya katika jamii.


Therapon University ni chuo cha masafa kinachotambuliwa kimataifa na kinajikita katika kutoa wahitimu wabobezi katika nyanja mbalimbali za Theolojia.


Wahitimu wametoa shukrani kwa elimu waliyoipata, wakisema itatumika katika kutumikia kanisa na jamii na Mahafali haya yanasherehekea mafanikio yao na kuwakumbusha wajibu wao katika huduma.






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso