Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk leo tarehe 04 Oktoba, 2024 ametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Wete na Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba yanayofanyika kwa siku mbili.
Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa sita wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utajumuisha mikoa mitano ya Zanzibar.
Uboreshaji wa Daftari kwenye maeneo hayo utaanza Oktoba 07 hadi Oktoba 13, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Washiriki wa mafunzo ambao ni Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Wete na Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakisikiliza nasaha za Makamu Mwenyekiti wa Tume. Washiriki hawa ndio watafanya kazi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika maeneo yao.
Washiriki wa mafunzo ambao ni Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Wete na Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakisikiliza nasaha za Makamu Mwenyekiti wa Tume. Washiriki hawa ndio watafanya kazi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika maeneo yao.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari leo Oktoba 04, 2024 ametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya za Magharibi A na B, mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar. Pichani akizungumza na Washiriki wa Wilaya ya Magharibi B mkoa wa Mjini Magharibi.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari leo Oktoba 04, 2024 ametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya za Magharibi A na B, mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar. Pichani akizungumza na Washiriki wa Wilaya ya Magharibi A mkoa wa Mjini Magharibi.
Washiriki wa mafunzo ambao ni Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar wakifuatilia nasaha za Mjumbe wa Tume. Washiriki hawa ndio watafanya kazi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika maeneo yao.
Washiriki wa mafunzo ambao ni Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar wakifuatilia nasaha za Mjumbe wa Tume. Washiriki hawa ndio watafanya kazi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika maeneo yao.
Washiriki hao wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kile cha kutunza siri.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira leo tarehe 04 Oktoba, 2024 ametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya wilaya ya Kusini, mkoa wa Kusini Unguja.
Washiriki wakisikiliza nasaha.
Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira akitamaza washiriki hao wakifanya mazoezi kwa ya kuunganisha vifaa vya BVR.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri leo Oktoba 04, 2024 ametembelea mafunzo kwa Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba yanayofanyika kwa siku mbili.
washiriki wakisikiliza nasaha kutoka kwa Mjumbe wa Tume.
Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akizungumza na Waandishi wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki (BVR) kutoka Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar leo wakati alipotembelea kituo hicho Aliyasema hayo leo tarehe 4 Octoba, 2024 akiwa katika kituo cha Mkwajuni TC kilichopo wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja.
Washiriki wakisikiliza nasaha kutoka kwa Mjumbe wa Tume.
Afisa Mwandikishaji ngazi ya Jimbo, Jaala Makame Haji wa Wilaya ya Kaskazini A akiwaapisha kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri kwa Waandishi Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki kabla ya kuanza mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyofanyika katika kituo cha Walimu Mkwajuni kilichopo Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja. Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza leo Octoba 04, 2024.
Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja. wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri.
No comments:
Post a Comment